November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC yatupa mapingamizi ya Tundu Lissu

Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeyatupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema dhidi ya wagombea wenzake wawili katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

Lissu aliwawekea pingamizi leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020, Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Miongoni mwa sababu alizoeleza Lissu zilizomfanya kuweka pingamizi ni makosa yaliyomo kwenye fomu za Rais Magufuli na Profesa Lipumba ikiwemo Rais Magufuli kuwasilisha picha zisizo sahihi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera amesema, baada ya kupokea mapingamizi aliwajulisha wahusika ambao walitoa utetezi wao.

Taarifa yote ya Dk. Mahera hii hapa:-

 

error: Content is protected !!