Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shibuda wa tatu kuteuliwa kugombea urais Tanzania
Habari za Siasa

Shibuda wa tatu kuteuliwa kugombea urais Tanzania

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua John Shibuda wa Ada Tadea kuwa mgombea urais wa Tanzania na Hassan Konde Kijongoo  kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Uteuzi wa wagombea hao umefanywa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage.

Jaji Kaijage amefanya uteuzi huo baada ya kujiridhisha Shibuda na Kijogoo wamedhi vigezo.

Shubuda amekuwa mgombea wa tatu kuteuliwa na NEC akitanguliwa na Rais John Pombe Magufuli wa Chgama Cha Mapinduzi (CCM).

           Soma zaidi:-

Wa pili kuteuliwa ni Leopard Mahona wa NRA kuwa mgombea urais wa Tanzania na Ally Khamis Hassan kuwa mgombea mwenza.

Vyama vilivyochukua fomu kuwania kuteuliwa kugombea urais ni 17 kati ya 19 vyenye usajiliwa kudumu.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!