Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwinyi ajibu mapigo ya Timu Maalim Seif
Habari za Siasa

Dk. Mwinyi ajibu mapigo ya Timu Maalim Seif

Dk. Hussein Mwinyi, Mgomnbea Urais Zanzibar (CCM)
Spread the love

WAKATI Timu ya Maalim Seif Sharif Hamad ‘ikishangilia’ uteuzi wa Dk. Hussein Mwinyi, kuwania urais Zanzibar, mwenye amesema ‘atateleza.’ Anaripoti Regina Mgonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ijumaa tarehe 11 Oktoba 2020, Dk. Mwinyi aliteuliwa kuwania urais Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati Maalim Seif akichukua fomu kugombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020, wakati akihojiwa na Kituo cha Azam TV, kuhusu mikakati yake kuelekea kwenye uchaguzi huo.

Dk. Mwinyi amesema, ushindi katika uchaguzi huo mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautokani na uzoefu wa mgombea, bali juhudi za mgombea katika kunadi sera zake kwenye kampeni.

Amesema, ili chama au mgombea achaguliwe na wananchi, inatakiwa chama kiwe na sera nzuri, na kwamba ana amini CCM kina sera nzuri zitakazoshawishi wapiga kura wakipe ushindi katika uchaguzi huo.

“Katika uchaguzi si uzoefu ni kujipanga kufanya kampeni sahihi, suala la kuweka sera nzuri ili zichaguliwe na wananchi. Tunaamini sera zetu ni nzuri, chama kiko vizuri,” amesema Dk. Mwinyi.

Aidha, Dk. Mwinyi amesema, kwenye uchaguzi huo, Wazanzibari watachagua mgombea mpya na kijana.

“CCM tunaingia na damu mpya, wenzetu wanaweka kila siku huyo huyo, wapiga kura vijana, hivyo wameweka kijana. Wao wanachobadilisha kwao ni jina la chama, ila wanachama ni walewale sioni kama kuna tatizo,” amesema Dk. Mwinyi.

Hoja kwamba hana umaarufu wa kisiasa visiwani Zanzibar, Dk. Hussein amesema, hoja hiyo haina mantiki na kwamba inatoka kwa mahasimu wake wa kisiasa.

Amesema, alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani kwa miaka 15, hivyo anaifahamu vizuri Zanzibar, na pia anafahamika visiwani humo

“Kuhusu mimi kutojulikana Zanzibar, sikuliona katika mtazamano huo, nilifikiri ni maneno yanayosemwa na baadhi ya watu wasiokuwa upande wangu. Nilihudumu Zanzibar katika Jimbo la Kwahani miaka 15, kusema sifahamiki si sahihi. Nafahamika vizuri,” amesema Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi amesema, endapoatafanikiwa kuwa Rais wa Zanzibar, atafuata nyayo za Baba yake, Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu, katika uongozi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!