Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa John Mnyika akimbia ubunge Kibamba
Habari za SiasaTangulizi

John Mnyika akimbia ubunge Kibamba

Spread the love

KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John John Myika, “ameutema rasmi” ubunge wake, katika jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea).

Mnyika ambaye amekuwa mbunge wa Kibamba ambayo ilikuwa sehemu ya jimbo la Ubungo, kwa miaka 10 mfululizo, hayumo katika orodha ya wanachama wa Chadema, waliopigiwa kura za maoni, kutaka kuteuliwa kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Hakuna taarifa zozote zinazoeleza sababu za mwanasiasa huyo, kutokugombea tena nafasi yake hiyo.

MwanaHALISI Online limeshindwa kumpata Mnyika kuzungumzia kutogombea kwake kwani simu yake ya kiganjani imekuwa ikiita pasina kupokelewa.

Hata hivyo, baadhi ya washindani wake  ndani ya Chadema wanasema, mbunge huyo ameamua kutokugombea nafasi yake hiyo, kwa kuhofia kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Wakati baadhi wakidai hivyo, taarifa zinasema, hatua ya Mnyika kujiweka kando katika kinyang’anyiro hicho, imetokana na kubanwa na majukumu ya nafasi yake ya ukatibu mkuu.

Mnyika alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho Desemba mwaka 2019 akichukua nafasi ya Dk. Vicent Mashinji ambaye jina lake halikupendekezwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho ili kuidhinishwa na wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho.

Katika mkutano wa kura za maoni uliyofanyika leo Jumanne, tarehe 14 Juni 2020, Ernest Mgawe, mwenyekiti wa Chadema katika jimbo la Kibamba, alitangazwa mshindi.

Mgawe alipata kura 30, kati ya 71 zilizopigwa. Wengine waliofuata nyuma ya Mgawe, ni Nemes Tarimo aliyepata kura  22 na Humphrey Sambo, ambaye alikuwa diwani wa Mbezi, aliyeambulia kura 19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!