Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sirudi nyuma – Maalim Seif
Habari za Siasa

Sirudi nyuma – Maalim Seif

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, visa vinavyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ni sawa na ‘kumpiga teke chura.’ Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar…(endelea).

Akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa chama hicho kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkoa wa Magharibi “B” kichama jimboni Mwanakwerekwe, mjini Zanzibar leo tarehe 14 Julai 202, Maalim Seif amesema, hato rudi nyuma kwenye mapambano ya haki Zanzibar.

“Hata wafanyeje, sitovunjika moyo. Katika mapambano hakuna kuvunjika moyo, ninawataka wanachama wetu wa ACT Wazalendo kutorudi nyuma katika mapambano ya kutaka haki,” amesema.

Mkutano huo ni muendelezo wa mikutano ya ndani anayoifanya katika ziara yake ya kwanza mikoani tangu alipochaguliwa mwenyekiti wa ACT Wazalendo mapema mwaka huu.

Tayari ametembelea mikoa yote miwili ya kisiwani Pemba na mikoa ya Kaskazini na Kusini Unguja.

“Nimeapa kuendeleza mapambano. Na kama wananisubiri nivunjike moyo, watasubiri sana,” alisema Maalim Seif ambaye amechukua fomu ya kuomba chama kimteue kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Alichukua fomu hiyo tarehe 5 Julai 2020, wiki moja tu baada ya kutangaza rasmi kuwa, ataendelea kugombea wadhifa huo katika uchaguzi mkuu.  Maalim Seif amegombea mara tano (1995, 2000, 2005, 2010, 2010).

“Wananchi wa Palestina hadi leo wanaendeleza mapambano… wala hawavunjiki moyo; basi na sisi tutapambana mpaka tutakapokuwa tumetimiza malengo ya kushika dola ya Zanzibar,” amesema.

Alikumbusha harakati za mapambano zilivyokuwa wakati wa kutaka Uhuru; baada ya mapinduzi ya Januari 1964 na pale yalipoibuka mapambano mapya ya kutaka kukomesha mfumo wa utawala wa chama kimoja.

“Wazanzibari tuna historia nzuri ya mapambano tunapotaka haki. Mfumo wa chama kimoja ulituacha taabani na ukalazimu watu kufanya kazi ya kutia presha kutaka mfumo wa vyama vingi kwa lengo la kupata mfumo utakaosaidia wananchi walio wengi,” alisema.

“Tulianza kuimarisha taasisi ya CUF iliyokuwa ikiogopwa sana na dola, lakini ulipandikizwa mgogoro na dola ya CCM hadi kumhalalisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti japokuwa alijuzulu mwenyewe Agosti 2015, akikitelekeza chama hicho karibu na uchaguzi mkuu.

“Bado ninaamini katika uchaguzi ule tuliwashinda, lakini wakubwa wa CCM na serikali zao wakasema ili ‘kuepuka fedheha ya kumpa Seif haki yake’ ni lazima apokonywe chama,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!