Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika atoa onyo wagombea ubunge, udiwani Chadema 
Habari za Siasa

Mnyika atoa onyo wagombea ubunge, udiwani Chadema 

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeonya watia nia katika kugombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, kutoleta mpasuko ndani ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020, na John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema, wakati anafungua mafunzo ya watia nia wa kugombea ubunge, udiwani na urais, katika Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam.

Leo Chadema imeanza rasmi utekelezaji wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.

 Uchukuaji fomu za kugombea ubunge, udiwani na uwakilishi litakoma rasmi tarehe 10 Julai mwaka huu, huku upande wa urais wa Zanzibar na Tanzania likifika tamati tarehe 19 Julai 2020.

Katibu huyo wa Chadema amesema, chama hicho hakitamvumilia atakayebainika kufanya vitendo vitakavyoleta mpasuko ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, Mnyika amesema, ili kuondoa makundi Chadema kitafuata misingi yote ya haki na kidemokrasia.

        Soma zaidi:-

“Niwaombe watia nia wa Pwani na kote nchini, mchakato wa uteuzi tuepuke kabisa isiwe chanzo cha migogoro na kutugawa. Sisi tutazingatia misingi yote ya haki na ya kidemokrasia. Hatutabagua mtu kwa hali yake ya kifedha jinsia,” amesema Mnyika.

Wakati huo huo, Mnyika amesema ni marufuku kwa mwanachama kujihusisha na vitendo vya rushwa.

“Ni marufuku kutoa fedha kwa njia yoyote, vyakula vinywaji au zawadi yoyote kwa wajumbe ili kupata kura. Kuwasafirisha wajumbe wa mkutano kwenye mkutano. Au kutoa ahadi zenye lengo la kulipa fadhila kwa wajumbe au wapiga kura kabla zoezi kukamilika,” amesema Mnyika.

Pia, Mnyika amesema, ni marufuku kwa watia nia kufanya kampeni za kuwachafua watia nia wenzao.

“Marufuku kusambaza taarifa zenye lengo la kukashifu mgombea, kufanya kampeni kwa kuhusisha udini au ukabila, anatakiwa kuzingatia masharti kuhusiana na muongozi dhidi ya rushwa,” amesema Mnyika.

Mnyika amewataka wajumbe watakaohusika na kuteua wagombea, wasiwapitishe watia nia watakaobainika kununua wapiga kura, kwa kuwa hawaamini.

Mnyika amesema, mwanachama yeyote wa Chadema anaruhusiwa kuchukua fomu hata kama hajaandika barua ya kutia nia ya kugombea.

“Uchukuaji huu hauhusu waliotia nia peke yao. Waliotia nia kabla wana uhuru wa kuchukua fomu.”

“Mwanachadema yoyote popote pale hata kama hajaandika barua ya kutia nia kwenye eneo lake. Anaruhusiwa kuchukua fomu ya kugombea na hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 3 A cha muongozo wa kutangaza kusudio la kuwania nafasi ya uongozi kwenye vyombo vya uwalilishi serikalini,” amesema Mnyika.

Kuhusu utiaji nia wa kugombea majimbo na kata zilizoko katika Kanda ya Pwani, Mnyika amesema, hadi sasa jumla ya wanachama 148 wametia nia kugombea ubunge na ubunge viti maalum na 691 wametia nia kugombea udiwani na udiwani viti maalum.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!