Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Tutashinda kwa kishindo udiwani, ubunge Dar
Habari za Siasa

Chadema: Tutashinda kwa kishindo udiwani, ubunge Dar

Halima Mdee
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimeweza kupata wagombea wa ubunge na udiwani, takribani asilimia 90 ya viti vyote vinavyogombewa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020, katika kongamano la watia nia wa ubunge, Kanda ya Pwani, linalofanyika katika ukumbi wa Lion, Sinza, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama hicho, Halima Mdee.

Amesema, Chadema kimefanikiwa kushinda majaribu yote, katika kipindi kigumu.

Mdee ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amesema, haikutarajiwa pamoja na vitisho vyote vya vyombo vya dola, bado chama hicho kimeshinda majaribu hayo.

Amesema, yeye binafsi atazunguuka nchi nzima, kuhakikisha mgombea wa upinzani katika kiti cha urais,  wabunge na madiwani, wanashinda uchaguzi huo.

Mdee alikuwa akizungumza wakati anamkaribisha Katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo.

Aidha, Mdee amesema, Chadema kitashinda majimbo yote ya jijini Dar es Salaam, kama kilivyoshinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

“CCM na tume yao, tangu kipindi cha Rais Benjamin Mkapa hakuna mpinzani alikuja kufanya kampeni akarudi nyumbani, akalala hafalu mkurugenzi wa uchaguzi akampigia simu njoo uchukue cheti chako hakuna,” amesema Mdee.

Mdee amesema, Chadema kitashinda kwa kishindo uchaguzi huo kwa kuwa CCM haina ushawishi kwa wananchi, kutokana na kushindwa kuongoza, ikiwemo kukuza uchumi wa wananchi.

Mdee amewashauri watia nia hao kufanya kampeni zitakazowashawishi wananchi wawachague, kwa kuwa ushindi wao utatokana na nguvu ya umma, itakayotumika kulinda kura zao.

“Kama tuliweza kushinda 2015, 2020 tunakwenda kuchukua nchi kiulaini. Mimi sikutangazwa Kawe tangu 2010 bila nguvu ya umma.”

“2015 niliingia bungeni kwa nguvu ya umma, kapigeni mzigo msiende kufanya majaribisho kapigeni mzigo kindakindaki wataenda kulinda kura na wewe, na hakuna polisi watakaotosha. Tucheze karata zetu vizuri ushindi upo nje nje,” amesema Mdee.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!