Tuesday , 14 May 2024
Home Kitengo Michezo Man Utd, Tottenham vitani leo
Michezo

Man Utd, Tottenham vitani leo

Spread the love

LIGI Kuu nchini England inaendelea tena leo tarehe 19 Juni, 2020 kwa mchezo kati ya Tottenham dhidi ya Manchester United ukiwa muendelezo wa Ligi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kila timu toka kurejea kwa ligi hiyo baada ya kusimama kwa muda wa miezi mitatu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.

Pambano hilo litakuwa la kuvutia kutokana na timu hizo kupishana pointi nne tu kwenye msimamo wa Ligi, ambapo Manchester United ina pointi 45, ikiwa ya tano kwenye msimamo, huku Tottenham ikiwa na pointi 41, nakushika nafasi ya sita kwenye msimamo.

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amesema kuwa mshambuliaji wake kinara Harry Kane atarejea kwenye mchezo wa leo baada ya kupona jeraha lake.

Huku kwa upande wa Manchester United inatarajia kupata huduma kutoka kwa kiungo wake Paul Pogba ambaye anarejea leo uwanjani baada ya kutoka majeruhi.

Kwenye mchezo wa raundi ya kwanza Manchester United aliibuka na ushindi wa mabao 2-1, na kuwa ndiyo mchezo wa kwanza Mourinho kupoteza akiwa kama kocha mkuu wa Tottenham.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

Michezo

Unakosaje pesa ukiwa na Meridianbet leo

Spread the love Alhamisi ndio hii sasa mteja wa meridianbet ambapo leo...

error: Content is protected !!