September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Profesa Mbarawa kada wa 10 kujitosa urais Z’bar

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akionesha begi lenye fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Spread the love

PROFESA Makame Mbarawa, Waziri wa Maji amekuwa mwanachama wa kumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyejitosa kuchukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Profesa Mbarawa amekabidhiwa  fomu hizo leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 na Cassian Gallo’s,  Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC idara ya Oganaizesheni Zanzibar katika Ofisi za CCM Kisiwandui, Ugunja Zanzibar.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Profesa Mbarawa, amewaomba Wazanzibar na Watanzania kumuombea kwa Mungu, ili akamilishe taratibu zinazofuata salama, ikiwemo utafutaji wadhamini 250 katika mikoa mitatu ya Zanzibar.

“Natamani nifanye hivyo (kuongea kuhusu sababu za kutia nia ya kugombea urais), lakini naomba leo tusiongee mengi sababu ninakwenda kazini,  tuombe Mungu atufikishe salama. Ninalowaomba tumuombe Mungu atusimamie, atufanyie wepesi,” amesema Prof. Mbarawa.

Profesa Mabarawa anakuwa kada wa kumi wa CCM kuchukua fomu hiyo, tangu zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu lianze tarehe 15 Juni 2020. Zoezi hilo ambalo linaenda sambamba na utafutaji wadhamini, linatarajiwa kufika tamati tarehe 30 Juni 2020.

Wengine waliokwisha chukua fomu ni; Mbwana Bakari Juma alikuwa mtu wa kwanza kufungua dimba hilo.

Balozi Ali Abeid Karume ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abei Aman Karume kisha akafuatiwa na Mbwana Yahaya Mussa ambaye mpaka sasa ndiye mwanachama kijana aliyejitosa kuchukua fomu.

Mtaalamu wa uchumi aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika tawala zilizipita visiwani Zanzibar, Omary Sheha Mussa alikuwa wan ne kuchukua fomu.

Watano katika kunyany’anyiro hicho alikuwa, Waziri wa Ujenzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar na Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.

Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) alikuwa wa sita kuchukua fomu kasha akafuatia Mohammed Jaffar Jumanne, Mkurugenzi wa Ushindani wa Biashara Halali Zanzibar.

Balozi Ali Karume

Wanane, alikuwa  Mohammed Hijja Mohammed na wa tisa akawa, Balozi Meja Jeneral mstaafu, Issa Suleimani Nassor.

Miongoni mwao na wale watakaoendelea kuchukua, wanawania kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye anamaliza kipindi chake cha utawala wa miaka kumi na kwa mujibu wa Katiba, hotogombea. 

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV

error: Content is protected !!