Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Michezo Man City yaipiga Arsenal ‘tatu mtungi‘
Michezo

Man City yaipiga Arsenal ‘tatu mtungi‘

Spread the love

MANCHESTER City imerejea vyema katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuishushia kipigo cha ‘tatu bila’ timu ya Arsenal. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ligi hiyo, imerejea jana Jumatano tarehe 17, 2020 baada ya kusimama kwa muda kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Hadi inasimamishwa, timu zilikuwa zimecheza michezo 29 isipokuwa Manchester City, Arsenal, Aston Villa na Sheffield United, zilizokuwa zimecheza mechi 28.

Timu hizo nne, zilicheza ili kukamilisha viporo hivyo ambapo mechi ya awali iliwakutanisha Aston Villa iliyowakaribisha Sheffield United ambapo mechi iliyomalizika bila kufungana.

Mechi hizo zote, zilichezwa zikiwa na mashabiki wachache sana ili kuchukua tahadhari ya maambukizo ya corona.

Kwa matokeo hayo, Aston Villa inayocheza Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, imebaki nafasi ya 18 kati ya timu 20 ikiwa na alama 26 huku Sheffield United wakiwa nafasi ya sita na alama zao 44.

Mtanange wa pili uliowakutanisha vijana wa Pep Guardiola katika dimba la Etihad, ilishuhudiwa Arsenal wakikubali kipigo hicho cha goli 3-0.

Kipigo kama hichohicho, walikipata katika mzunguko wa kwanza walipokutana.

Raheem Sterling, ndiye aliyefungua milango ya Arsenal, dakika ya 45 kipindi cha kwanza, baada ya kupiga shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari ‘miguu 12’ na kwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa wa vijana wa kocha, Unai Emery, Bernd Leno akishindwa afanye nini.

Timu hizo zilikwenda mapumziko huku Man City wakiwa mbele kwa goli hilo moja.

Hata hivyo, sifa zimwendee kipa wa Arsenal, Bernd Leno ambaye aliokoa michomo ya vijana wa Man City waliokuwa na uchu wa mabao tangu awali.

Kipindi cha pili kiliporejea, iliwachukua dakika tano, Man City kupata bao la pili lililofungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 50 kwa mkwaju wa penati.

Penati hiyo, ilipatika baada ya beki wa Arsenal, David Luiz kucheza rafu ya kumshika begani akiwa ndani ya ‘box’ mshambuliaji wa Man City, Riyad Mahrez.

Kutokana na faulo hiyo, mwamuzi alimzawadia kadi nyekundi Luiz hivyo kuwafanya Arsenal kucheza pungufu.

Kutokana na wachezaji kadhaa kuumia, ziliongezwa dakika 11 na ndani ya kipindi hicho yaani dakika ya 91, Phil Foden akaiandikia bao la tatu Man City kwa shuti kali ndani ya ‘miguu 12’ baada ya kutokea
piga nikupige.

Kwa ushindi huo, Manchester City imefikisha alama 60 ikishika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na majogoo ya Anfield, Liverpool yenye alama 82.

Kipingo hicho kwa Asernal, kumeifanya kubaki na alama zake 40 ikiwa nafasi ya tisa ya msimamo huo wenye timu 20.

Ligi hiyo itaendelea kesho Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 kwa Tottenham wanaofundishwa na Jose Mourinho kuwakaribisha mashetani wekundi, Manchester United ambayo inanolewa na kocha, Ole Gunnar Solskjaer.

Pia, kutakuwa na kipute kati ya Norwich City itakayowakaribisha Southmpton.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!