Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Uchaguzi mkuu 2020: Wafadhili waipa mamilioni THDRC
Habari Mchanganyiko

Uchaguzi mkuu 2020: Wafadhili waipa mamilioni THDRC

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Spread the love

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema, utaendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa habari ya namna watakavyofanya kazi zao kwa usalama pamoja na kuwajengea uwezo mawakili wanaotetea haki za binadamu. Anaandika Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa na Mratibu wa mtandao huo, Onesmo Olengurumwa wakati akisaini mkataba wa Dola za Kimarekani 120,000 ambazo ni sawa na Sh. 277 milioni na Shirika la wafadhili la Initiative for Eastern Africa (OSIEA) kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo.

Olengurumwa amesema, mafunzo hayo yana lengo la ushirikiano na Serikali, Mahakama na kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji kazi kwa watetezi wa haki za binadamu.

Amesema, mkataba huo ni wa kipindi cha mwaka mmoja ambao ni kama nyongeza kwakuwa shirika hilo ni wadau wakwanza waliowapa fedha za uanzilishi wa taasisi tangu 2012 hadi leo wamekuwa wakifanya kazi pamoja.

“Hizi ni kama fedha za nyongeza ya fedha ambazo tumeendelea kuzipokea kutoka kwao kwa miaka yote kila mwaka, kwa utaratibu tuliouzoea tunapopata fursa, tunaposaini mkataba ni vyema tukatoa taarifa kwa wadau wenzetu juu ya washirika wetu tunavyoshirikiana nao,” amesema.

Amesema shughuli za watetezi wa haki za binadamu zinakuwa katika mazingira magumu hasa katika kipindi cha uchaguzi hivyo fedha hizo zitasaidia kuboresha shughuli za kuwajengea uwezo watetezi wa haki za binadamu katika masuala ya usalama na utetezi.

Pia, kusimamia sheria mbalimbali na kuwagusa mawakili wanaotetea haki za binadamu katika maeneo ya kusimamia kesi za uchaguzi pamoja na watetezi waangalizi wa uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!