Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mapambano ya corona: Bunge kumpongeza Rais Magufuli
Habari za Siasa

Mapambano ya corona: Bunge kumpongeza Rais Magufuli

Rais John Magufuli
Spread the love

BUNGE la Tanzania, linatarajia kupitisha azimio la kumpongeza Rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli, kwa namna alivyoliongoza Taifa katika Mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020 zilizotolewa na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai inaonyesha azimio hilo litawasilishwa bungeni leo.

“Azimio la Bunge la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli, kwa namna alivyoliongoza Taifa katika Mapambano dhidi  ya Janga la Ugonjwa wa Corona (COVID-19),” inasomeka kwenye orodha za shughuli za Bunge

Kwa mujibu wa taarifa za Serikali ya Tanzania kuhusu hali ya maambukizo ya corona nchini Tanzania zinadai yamepungua.

Bunge la Tanzania

Mgonjwa wa kwanza wa corona alitangazwa tarehe 16 Machi 2020 na mpaka jana Jumatatu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa mkoani Tanga alisema, wagonjwa wamepungua na hivi karibuni watatangaza kutokuwepo kwa mgonjwa yoyote wa corona.

Tayari vyuo vilivyokuwa vimefungwa tangu tarehe 18 Machi 2020 vimefunguliwa kuanzia tarehe 1 Juni 2020 pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita.

Wanafunzi wa kidato cha sita wanajiandaa na mitihani yao ya taifa kuanzia tarehe 29 Juni hadi 16 Julai 2020 na matokeo yanatakiwa kutoka kabla ya tarehe 31 Agosti 2020.

Hivi karibuni, Rais Magufuli alisema kwa hali inavyoendelea, anafikiria kufungua shule za msingi na sekondari ili masomo yaweze kuendelea kama kawaida.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!