October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ni vita ya fedha GSM Vs Mo

Spread the love

‘VITA’ ya fedha inakwenda kutikisha msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (2020/21). Ni baada ya vilabu vikubwa viwili nchini – Klabu Simba na Yanga – kupania kusajili wachezaji wakali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Klabu za Simba na Yanga tayari zimetoa maneno ya majigambo, kwamba vitasajili wachezaji wenye viwango bila kujali pesa ili kuingia kwenye msimu ujao wakiwa kamilifu.

Ikiwa ni siku chache baada ya wafadhili wa Yanga (GSM) kutangaza kuvunja benki kwa usajili wa kishindo, mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji (MO) amesema, ‘nitanunua mchezaji yeyote atakayehitajika.’

Mo ambaye anamiliki asalimia 49 katika klabu hiyo baada kubadilishwa Katiba na muundo na wa uendeshaji tarehe 3 Disemba 2017, ameandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa twitter huku akiwahakikishia wana Simba, kuwa hakuna mchezaji atayeondoka.

Kauli ya Mo imetolewa ikiwa ni siku chache baada ya GSM kupitia Hersi Said, Mkurugenzi wa Oparesheni kusema, mara baaada ya msimu kumalizika, watafanya usajili wa kishindo kwa kuleta wachezaji bora ndani ya Bara la Afrika. GSM wamesema, miongoni mwa malengo ya kwa sasa ni kushinda kombe Shirikisho la Azam.

Kwa upande wa Simba, tangu kuja kwa MO kama mwekezaji, timu hiyo imeonekana kutulia na kuwa na mafanikio kwa muda mfupi ambapo imeshinda mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo.

Timu hiyo pia ilifikia hatua ya robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika, katika msimu uliomalizika.

Lakini pia, ujio wa GSM ndani ya Yanga umeleta mabadiliko makubwa kwa kuisadia timu hiyo kifedha katika kusimamia mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji.

GSM wamekuwa wakihudumia kambi sambamba na kutoa mishahara kwa wachezaji na makocha, kusaidia kwenye usajili wa wachezaji.

Klabu hizo mbili kwa sasa zinajiandaa na michezo ya Ligi Kuu ambayo inarejea mwisho wa wiki hii, kikosi cha Yanga kitakuwa mkoani  Shinyanga kuikabili Mwadui FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, mabingwa watetezi ‘Simba’ itashuka dimbani tarehe 14 juni 2020 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuikabili Ruvu Shooting.

error: Content is protected !!