Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yajitosa Urais Zanzibar, yatoa siku 10
Habari za Siasa

Chadema yajitosa Urais Zanzibar, yatoa siku 10

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimefungua milango ya wanachama wake wanaotaka kuwania urais wa Zanzibar,  kuandika barua kwenye ofisi ya naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zanzibar kuanzia leo Juni 6 hadi 15, 2020 saa 10:30 jioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Hii ni mara ya kwanza kwa Chadema, kutangaza rasmi kuweka mgombea katika nafasi ya Urais.

Hayo yamesemwa na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanziba, wakati akizungumza na wanahabari visiwani humo leo Jumamosi tarehe 6 Juni 2020, kuhusu maandalizi ya chama hicho, kuelekea uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na wawakilishi.

“Leo hii chama chetu kinafungua milango kwa wanachama wake wote wenye sifa, uwezo na maadili kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya Chadema kuhusu muongozo wake wa kusudio la kutangaza nia wajitokeze kuomba kugombea Urais Zanzibar,” amesema Mwalimu.

Kuanzia leo hadi tarehe 15 Juni 2020 muda wa mwisho ni siku 10 tu kwa wanachama wa Chadema watatumia kutangaza nia hizo na kuandika barua.

Aidha, Mwalimu amewataka wanachama wa chama hicho walioko nje ya nchi kwa sasa, kuwasiliana na ofisi yake ili wapewe utaratibu wa kuwasilisha kusudio lao la kugombea Urais Zanzibar kupitia Chadema.

“Kwa wale ambao taarifa hizi za kutangaza nia zitawakuta nje ya Zanzibar, wanaruhusiwa kufanya mawasiliano na ofisi Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ili tuweze kuwawekea utaratibu upi wa kuweza kuwasilisha kusudio lao hilo la kugombea Urais Zanzibar kupitia Chadema,” amesema Mwalimu.

Mwalimu amesema, “chama kimejipima na kutafakari kwa kina na kimeona kwamba sasa ni wakati muafaka kuwapa nafasi wanawachama wake wenye ndoto na uwezo wa kugombea nafasi hiyo kutimiza ndoto zao.”

Amesema, pamoja na tangazo hilo, chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, “kipo tayari kuendeleza ushirikiano na vyama na kulinda  nia na shabaha ya ushirikiano huo bila kuathiri malengo ya vyama vyetu kwa masilahi ya kila Mzanzibar katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.”

Hatua hiyo ya Chadema kufungia milango ya utiaji nia ya kugombea urais visiwani Zanzibar inajiri siku kadhaa, baada ya John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho, kufungua milango hiyo kwa nafasi ya Urais wa Tanzania.

Tarehe 3 Juni 2020, Mnyika alifungua milango hiyo na kuwataka wenye nia kuandika barua ofisi yake na mwisho ni tarehe 15 Juni 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!