Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mchungaji Msigwa amtangulia Lissu ‘urais’ Chadema 
Habari za SiasaTangulizi

Mchungaji Msigwa amtangulia Lissu ‘urais’ Chadema 

Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini
Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini tayari amefungua pazia la kugombea urais ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mbunge huyo amefikisha barua yake katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.

Amefanya hivyo ikiwa ni siku mbili kupita baada ya Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kueleza dhamira ya kuomba ridhaa ya chama chake kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Lissu aliieleza MwanaHALISI ONLINE kwamba alikuwa anasubiri milango ya kugombea urais ifunguliwe katika chama chake.

“Kama mwanachama mtiifu wa Chadema, nilikuwa nasubiri uongozi wa chama unaohusika, utoe baraka zake kwa wanachama kuanza mchakato wa uchaguzi,” alisema Lissu na kuongeza:

“Nilikuwa nasubiri baraza za chama, nitaandika barua ya kuomba ridhaa ya chama changu nigombee urais.”

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020 Mchungaji Msigwa amesema, amejipima na kuona ana uwezo wa kuliongoza taifa, hivyo amewasilisha barua yake kuomba ridhaa ya chama chake kumteua.

“Nimewasilisba barua yangu kwa Katibu Mkuu kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais, nimejipima na nimeona nina uwezo wa kuliongoza taifa,” amesema Mchungaji  Msigwa na kuongeza “nisipopita nitamuunga mkono yule atayepitishwa na chama lakini nimeona nina uwezo.”

Alipoulizwa kama yupo tayari kuliachia Jimbo la Iringa Mjini, amesema kwamba ndani ya chama hicho, mchakato wa kwanza ni kumtafuta mgombea rais na iwapo atashindwa, atarudi jimboni.

“Urais na ubunge ni michakato miwili tofauti, tunaanza urais na kisha ubunge. Na kama akipitishwa mtu mwingine, mimi nitarejea kutetea jimbo langu,” amesema Mchungaji Msigwa.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho alitangaza kufunguliwa kwa milango kwa wanachama wa chama hicho, wanaotaka kuwania urais kuandika barua kwenye ofisi yake.

Alisema, milango hiyo imefunguliwa kuanzia tarehe 3 Juni hadi 15 Juni mwaka huu na kwamba, baada ya hapo, watakaokuwa wamejitokeza, watapelekwa kamati kuu ya chama hicho kwa hatua zaidi za ndani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!