November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yajiimarisha kurejea Ligi Kuu Bara

Boniface Mkwasa

Spread the love

KIKOSI cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi yake kwenye viwanja vya chuo cha Sheria, Jijini Dar es Salaam katika hatua ya kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho inayotarajia kuanza hivi karibuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Ligi hiyo inayotarajia kuendelea Juni 13, 2020 baada yakusimama kwa takribani miezi miwili kutokana na mlipuko waugonjwa wa Covid 19.

Yanga ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha wao msaidizi, Boniface Mkwasa amesema kuwa wachezaji wake wanaendelea vizuri toka walipoanza mazoezi katika siku saba zilizopita lichaya baadhi yao kuongezeka uzito kidogo.

Wachezaji wote wamerejea mazoezini na wanaendelea kujiandaa vizuri licha ya baadhi yao kuongezeka uzito kidogo lakini tumewapa program maalumu kwa kupunguza uzito ili warejee kwenye hali yao ya kawaida,” alisema Mkwasa.

Aidha kocha huyo aliongezea kuwa siku ya Jumapili wanatarajia kucheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ili kuwaweka wachezaji wake kwenye utimamu wa mwili baada ya mapumziko ya muda mrefu.

Timu hiyo itashuka dimbani Juni 13, 2020 kwenye uwanja wa CCM Kambarage kuikabili Mwadui katika muendelezowa micheo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

error: Content is protected !!