Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Wachezaji Manchester warejea, wapimwa Corona
Michezo

Wachezaji Manchester warejea, wapimwa Corona

Spread the love

BAADHI ya nyota ya Manchester United jana walionekana kurejea kwenye eneo la viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo (Carrinton) kwa ajili ya kufanya vipimo vya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na kirusi aina ya Corona (Covid-19) kabla ya kuanza rasmi mazoezi kwa ajili ya kuendelea na michezo iliyosalia ya Ligi Kuu England ambayo ilisimama kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa, Manchester … (endelea).

Mshambuliaji Marcus Rashford, Paul Pogba, David Degea, Anthonio Martial, na beki Phili Jones ni baadhi ya nyota waliofika kwenye viwanja hivyo huku wakipishana kwa muda wa dakika 15 kila mmoja kuwasili hapo kutokana na utaratibu uliowekwa na uongozi wa klabu hiyo katika kujilinda dhidi ya Corona.

Baada ya kuwasili hapo wachezaji hao walichukuliwa vipimo vya Covid-19 kama utaratibu ulivyo na kama matokeo yakiwa hasi ndio wataruhusiwa kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu na mashindano mengine.

Mazoezi hayo ambayo yanatarajia kuanza hivi karibuni, wachezaji watapaswa kufuata mwongozo wa chama cha soka nchini hapo ambao umeutoa kwa klabu ya mazoezi na baada ya mazoezi kama kwenye makundi madogo madogo, kutochezeana rafu na kufanya mazoezi kwa muda mfupi.

Ligi hiyo ilisimamishwa mwezi Machi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona na inauwezekano kurudi tena Juni, mwaka huu kama mwenendo wa ugonjwa huo utakuwa mzuri kama ilivyoanisha serikali ya nchi hiyo.

Mpaka ligi hiyo inasimama tayari ilishachezwa michezo 29 kwa kila timu huku Liverpool ikiwa kinara kwenye msimamo baada kuwa na alama 82, huku Manchester United ikishika nafasi ya tano kwa kuwa na alama 45.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!