Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Mtalii hatowekwa karantini
Habari za Siasa

JPM: Mtalii hatowekwa karantini

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amemwagiza Dk. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Utalii na Injinia Isack Kimwelwe, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano kuruhusu ndege za utalii kutoka nje, na kwamba mtalii hatowekwa karantini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Msimamo huo ameutoa leo tarehe 17 Mei 2020, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ushirika wa Chato, alipokwenda kufanya ibada.

“Mpaka ninapozungumza hapa, kuna masharika ya ndege ambayo siwezi kuyataja yashabook (orodhesha) watalii wengine mpaka mwezi wa nane, ndege zimejaa kwa ajili ya kuja Tanzania kuanza kutalii, wanakuja kwa sababu wanaujua ukweli wanakuja kwa sababu Tanzania ni pazuri,” amesema.

Amesema, watalii hao wakifika nchini, hawatawekwa karantini isipokuwa watapimwa joto lao la mwili kisha kuruhusiwa.

“…nimeishatoa maagizo kwa Waziri wa Maliasili na Waziri wa Uchukuzi waruhusu hizo ndege ziingie, na wala hawatawaweka karantini. Wakishafika hapa, akishapimwa akakutwa na temperature (joto) ipo kawaida, hana dalili za corona aendee akaangalie wanyama huko…,”amesema na kuongeza:

“Hatuwezi sisi kama taifa huru tukakubali corona itawale, Mungu wetu atatawala lakini corona haitatawala.… Tukiufanya uchumi wetu ukalala, hata mishahara hatutalipa.”

Rais Magufuli amewataka Watanzania kuondoa na hofu, kwa kuwa hofu ni ugonjwa mbaya kuliko corona “nitoe wito kwa Watanzania, kuna maneno mengi yaliyotiwa chumvi, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko corona.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!