Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Corona haihitaji kiburi
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Corona haihitaji kiburi

Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameeleza kuwa mapambano dhidi ya gonjwa la Corona, hayahitaji mzaha au kibri. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea). 

“Janga hili halihitaji masihara. Halihitaji mizaha wala halihitaji usiri katika kulikabili,” ameeleza Mbowe wakati akizungumza na wananchi kupitia mitandao ya kijamii, leo Jumapili, tarehe 17 Mei 2020.

Alisema, kufuatia msimamo huo, ndio maana Kamati Kuu (CC) ya chama chake, imetaka wananchi kuweka tofauti za kisiasa pembeni, na kutoruhusu chuki za kisiasa, kiburi cha madaraka na mamlaka, katika kupambana na vita hiyo.

Kwa mujibu wa Mbowe, ripoti mbalimbali za kimataifa na tafiti za kisayansi, zinaonyesha kuwa janga la Corona sio jambo la kuisha haraka. Amesema, Corona ni janga ambalo taifa linapaswa kujipanga kuishi nalo kwa muda mrefu.

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Kilimanjaro amesema, “hakuna njia ya mkato, ni lazima taifa kufikiria kwa mawanda mapana katika kulikabili janga hili.”

Amewataka wananchi kutambua kuwa ugonjwa huo utakuwa na athari kubwa katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na itachukua muda mrefu kukabiliana na athari zake.

Amesema, “…tupende tusipende, uchumi wa nchi yetu utaporomoka; na kutakuwa na ugumu mkubwa kwa serikali kutekeleza bajeti yake.

“Hata mipango ya biashara ya mashirika na kampuni za ndani na wawekezaji wa nje, nayo itayumba kimtaji, na hivyo kusababisha makampuni mengi kufilisika.”

Akizungumzia sekta ya ajira, Mbowe amesema, “watumishi wengi wa sekta binafsi, watapoteza ajira zao, na hivyo kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira mara dufu.”

Hata hivyo, Mbowe amesema, chama chake kimesikitishwa na namna ushauri unaotolewa na vyama pinzani nchini, unavyopokelewa kama ugomvi.

Amesema, Chadema kimeweka rekodi kwamba katika vita dhidi ya Corona, kulihitaji ushirikishwaji, uwazi, umoja na ukweli.

“Tuliisihi sana serikali isihodhi janga hili kwani inahitaji nguvu na mshikamano wa pamoja kwa kuwa, ni suala la uhai na kifo kwa kila mmoja wetu,” amesisitiza.

Amesema, chama chake kilisisitiza sana umuhimuwa kupima kwa haraka zaidi, ili waathirika waweze kujulikana na kisha watengwe vizuri kama njia muhimu ya kupunguza maambukizi mapya.

Amesema, “tulishauri sana serikali kuacha kuficha au kupunguza idadi ya waathirika na hatimaye vifo, tukiamini ukweli na ukubwa wa janga hili kujulikana kutaongeza ufahamu wetu na umakini.”

Amesema, kwa sasa, kama wataanza kubishana zaidi kwenye vyombo vya habari, inawezekana kuanza kutengeneza mpasuko. Hivyo, amewataka wananchi kujikinga wenyewe kwa kuwa ndio wanaopaswa kuwa mstari wa mbele.

Akizungumzia mhimili wa Bunge, Mbowe alidai kuwa kutokana na kasi ya kusambaa kuwa kubwa zaidi hata kuutingisha mhimili huo.

Lakini baada ya kuona ushauri wetu hautiwi maanani, tarehe 1 mwezi Mei 2020, chama chetu kiliagiza wabunge wake kujilinda na kuwalinda wengine kwa kwenda karantini kwa siku 14 huku tukisihi Bunge zimaikijumuisha watumishi kutafakari uwezekana wa kujiweka karantini na kupima.

Tulitoa ushauri huo kwa wabunge  wetu nia njema  tukiamini kwamba wabunge wetu wamekuwa katikati ya bunge ambalo limepata mitikisiko …kwa bahati mbaya sana mapokeo ya ushauri wetu yalipokelewa very negative (mapokeo hasi).

Amesema, “nasikitika kwa namna ambavyo ushauri wetu wenye nia njema kabisa ulivyopokelewa hususan kwa viongozi wetu wakuu wa mhimili  hasa Bunge na serikali. Kilichoonekana ni kwamba tunatangaza uhasama wa wazi; tunatangaza malumbano na mapambano ya kuoneshana nani mkubwa na nani mwenye nguvu.

“Janga la Corona halimjali mwenye nguvu au udhaifu wote tunastahili kuheshimiana  na kuona kipi ni bora. Yawezekana usipende ushauri, lakini hata kuopokea au kuukata ushauri unaweza kuupokea kwa staha na maisha yakaendelea na watu tukaendelea kuheshimiana.

“Tangu nilipotoa hotuba yangu na usahuri wa chama chetu kujiweka karantini  kama ilivyoshauriwa na WHO (Shirika la Afya ulimwenguni), kwamba mmoja wenu au kukawa na hisia ya mmoja  kuambikizwa au mmoja wenu kuambukizwa, ushauri ni kundi zima kujitenga.

“Lakini baada ya hapo kiongozi wa Bunge, Mheshimiwa Spika Job Ndugai, ametumia majukwaa mbalimbali ya nje na ndani ya Bunge kunishambulia na kunidharirisha mimi binafsi;  kadharirisha viongozi wenzangu, wabunge wa chama chetu kwa lugha zisizokuwa na staha baada kujadili ushauri tulioutoa.

“Badala ya kuiona nia yangu njema, wametumia mamlaka yao ya ofisi ya umma  kutudharirisha huku taifa likiindelea kushuhudia roho za watu wasiokuwa na hatia zikipotea kwa kasi.”

Mbowe anasema, Spika Ndugai anadai tunachukulia kila kitu kisiasa; sisi tunakiri kama chama wajibu wetu ni wa kisiasa na ndio unaotupa uhalali sisi kama Chadema kuitwa chama cha siasa; na sio dhambi sisi kama chadema kuitwa wanasiasa.

“Tunapenda kuwakumbusha viongozi wetu kuwa siasa ni maisha ya kila siku na yanagusa binaadamu na hata wao kila wanalofanya siasa tofauti yao watawa na sisi watawaliwa ni kuwa maamuzi yao wasiokuwa makini huumiza wengi na hatimaye huua wengi wasiokuwa na hatia.

“Spika kila akitaka kuahirisha Bunge lazima apande na Mbowe, sasa Spika ni baba na mzazi kama ilivyo wengi. Wanakazana wanaotupaka sifa za uovu kama alivyo mzazi nami ni mzazi; ni baba nina watoto ninawaongoza… anajua vizuri sana kwamba tumekutana bungeni miaka 20 iliyopita, tumefanya kazi chini ya mheshimiwa Pius Msekwa.

“ …tumehudumu wote kamati za kanuni kwa miaka kumi mfululizo.. na  wengine pengine hawajui kuwa Mheshimiwa Spika ameseoma Kibaha Sekondari nami nimesoma Kibaha Sekondari kwa hiyo ni school mate wangu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!