Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Wachezaji EPL wagoma kurudi mazoezini
Michezo

Wachezaji EPL wagoma kurudi mazoezini

Sergio Kun Aguero
Spread the love

PAMOJA na Serikali Uingereza kutoa taarifa kuwa kuna uwezekano michezo ikarejea Juni Mosi, 2020 lakini baadhi ya wachezaji wa klabu za Ligi Kuu wamegomea makocha wao, kurejea mazoezini siku ya Jumatatu kutokana na hofu ya ugonjwa wa Covid 19. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Baadhi ya wachezaji ambao wameonesha hawako tayari kurudi kwenye viwanja vya mazoezi siku hiyo ni mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Sergio Kun Aguero, beki wa kushoto wa Newcastle, Danny Rose na kiungo wa West Ham United, Manuel Lanzini.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Daily Mail limeeleza kuwa wachezaji hao wamewaambia makocha wao kuwa hawako tayari kurudi mazoezini kwa sasa, kutokana na janga la ugonjwa wa Covid 19 kupitia makundi kwenye mtandao wa Whatsapp.

Hata hivyo mtandao huo, umeripoti kuwa katika Saa 48 zijazo baadhi ya klabu zitafanya mkutano na wachezaji wao kwa njia ya video ili kuwapa maelekeo ya kujilinda dhidi ya virusi vya Corona watakaporejea kwenye viwanja vya mazoezi.

Hivi karibuni umoja wa klabu za Ligi Kuu nchini humo ulikubaliana kumalizia michezo iliyosalia ya Ligi Kuu kwa kuchezwa katika baadhi ya viwanja bila ya mashabiki.

Mpaka ligi hiyo inasimamishwa tayari kila timu ilishacheza michezo 29, huku Liverpool ikiwa kileleni kwenye msimamo ikiwa na pointi 82, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 58 huku Norwich ikishika mkia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!