Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Weijia Jiang, mwandishi aliyemtoa Rais Trump kwenye ‘reli’
Habari MchanganyikoKimataifa

Weijia Jiang, mwandishi aliyemtoa Rais Trump kwenye ‘reli’

Spread the love

MKUTANO wa Rais wa Marekani, Donald Trump na wanahabari, umevunjika baada ya rais huyo kuulizwa maswali yaliyomchefua. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

 Mkutano huo ulifanyika jana Jumatatu tarehe 11 Mei 2020, kwenye viwanja vya Rose Garden ndani ya Ikulu ya Marekani, ambapo swali la mwandishi wa kituo cha habari cha CBS, Weijia Jiang lilimtibua Trump.

Trump aliitisha mkutano huo ili kueleza namna Marekani inavyochukua hatua katika kudhibiti virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona (COVID-19).

Ilikuwa saa 11:15 kwa majira ya Washington ambapo Trump aliruhusu maswali baada ya kuelezea hatua na mikakati yake dhidi ya corona.

Jiang alipopata nafasi, alimuuliza Trump kwamba, siku zote amekuwa akiieleza dunia kwamba, wanafanya vizuri katika kupima watu walioathirika na virusi hivyo kuliko taifa lolote dunia, lakini wamarekani waanaendelea kuambukizwa na kufa, nini maana yake?

Alisema “mara nyingi umekuwa ukisema kwamba Marekani inafanya vizuri kuliko taifa lolote kuhusu kupima watu kama wana virusi,” wakati akiuliza swali hilo Trump alitikisa kichwa akionekana kukubaliana naye.

Jiang ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya China aliendelea na swali lake, “inakuweka katika nafasi gani kama kila siku Wamarekani wanaendelea kufa na tunaendelea kushuhudia maambukizi mapya?”

Swali hilo lilimchefua Trump ambaye alijibu “watu wanakufa kila mahali,” aliendelea kujibu “labda swali kama hili unapaswa kuiuliza China.”

“Usiniulize mimi, iulize China swali hilo, sawa?…kama utaendelea kuniuliza maswali ya namna hiyo, unaweza kupata matokeo  usiyotarajia kabisa.”

Baada ya kumpa jibu hilo Jiang, Trump alitoa nafasi kwa mwandishi mwingine kuuliza swali, hata hivyo Jiang alisogelea tena kipaza sauti na kuendelea kumuuliza “Mheshimiwa kwanini jibu hilo unalielekezea kwangu?”

“Sio  kwako tu,” alijibu Trump na kuendelea “jibu hilo ni kwa mtu yeyote anayeuliza maswali ya kipuuzi kama lako.”

Jiang alimng’ang’ania Trump kwamba “hili sio swali la kijinga.” Wakati mwandishi hiyo akiendelea kwenye kipaza sauti, tayari Trump alikuwa amejielekeza kwa mwandishi mwingine.

“Swali lingine?” aliuliza. Kabla ya kumruhusu mwandishi wa CNN, Kaitlan Collins ambaye alikuwa amesimama nyuma ya Jiang. “Sawa, endelea wewe hapo nyuma,” alisema.

Collins alipofika kwenye kipaza sauti, alisema “nina maswali mawili.”

Trump alisema ‘hapana’ sio wewe, “tunaendelea hapa mbele,” alisema Trump.

“…lakini ulinichagua mimi. Nina maswali mawili” Trump hakumsikiliza na aliuliza mwandishi mwingine kama ana swali. “Mwingine, mwingine tafadhali,” alisema Trump.

Collins alibaki kwenye kipaza sauti akisisitiza kwamba aliitwa yeye “bali uliniita mimi.” Trump alimjibu “ndio lakini hukuitikia, na sasa namwita binti mwingine pale nyuma.”

“Lakini nataka nimalizie,” Collins alimwambia Trump akiwa kwenye kipaza sauti. Kabla ya kuendelea zaidi Trump alisema “mabibi na mabwana, nawashukuru” kisha akageuka nyuma na kuondoka.

Vyombo mbalimbali vya kimataifa vimeeleza, kinachofanya na Trump ni muendelezo wa chuki zake dhidi ya vyombo vya habari hasa tangu aanze kuzungumzia mwenendo wa kuenea kwa virusi vya corona Marekani.

Trump amekuwa hapendi kuulizwa maswali makali kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19 yanayofanywa na serikali yake, ambapo amekuwa akitoa majibu yasiyoridhisha kwa waandishi pale wanapohoji zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!