Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vita dhidi ya Corona: Wanywa bia baa wapigwa ‘stop’
Habari Mchanganyiko

Vita dhidi ya Corona: Wanywa bia baa wapigwa ‘stop’

Spread the love

SOPHIA Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, amepiga marufuku mikusanyiko ya watu katika baa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kudhibiti maambukizi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mjema ametoa marufuku hiyo jana tarehe 17 Aprili 2020, na kuelekeza wamiliki wa baa hizo kuhakikisha wateja wao wanaonunua bia, wanakwenda kunywea nyumbani.

Mjema amesema mtu yeyote atakaye kiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

“Waendesha baa mnaelekezwa kuwa vinywaji vitauzwa na mnunuzi atapaswa kunywea nyumbani, na sio kwenye baa. Ni wajibu wa kila mmoja kuzingatia maelekezo haya kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mmiliki, muendeshaji na mtu yeyote atakaye onekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa,” amesema Mjema.

Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya COVID-19, ikifuatiwa na Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, jiji hilo lina wagonjwa wapya 38 kati ya wagonjwa 53 walioripotiwa jana katika mikoa saba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!