Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Hakimu amgomea wakili wa Mbowe
Tangulizi

Hakimu amgomea wakili wa Mbowe

Viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

THOMAS Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam amegomea ombo la wakili wa Freeman Mbowe na wenzake, la kuomba siku 21 za maandalizi ya ushahidi. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na wenzake wanane, wanakabiliwa na tuhuma za kufanya uchochezi kwenye shitaka namba 221/2018 katika mahakama hiyo.

Wakili Kibatala aliiomba mahakama hiyo siku 21 kwa ajili ya kufanya maandilizi ya kupeleka utetezi, hata hivyo leo tarehe 21 Oktoba 2019, Hakimu Simba alisema ‘haiwezekani’ upande wa utetezi kupewa siku 21 na badala yake amewapa siku 14.

Mbali na kutoa siku 14 Hakimu Simba amesema, ombi lingine la Wakili Kibatala la kuomba kielelezo namba P4 ambacho ni (Min Div) – mbili zilizotolewa mahakamani hapo na shahidi wa saba wa serikali Koplo Charles, haliwezekani.

Hakimu Simba amesema, kielelezo hiko hakiwezi kutolewa nje ya mahakama, isipokuwa kitolewa kwa ajili ya kuoneshwa chini ya utawala wa mahakama kwenye ukumbi wa mahakamani na usimamizi wa mahakama kama ilivyokuwa kwa upande wa Jamhuri.

Viongozi tisa wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho Taifa, wanakabiliwa na kesi ya uchochezi namba 221/2018 kwenye mahakama hiyo ambayo iliwakuta na na kesi ya kujibu.

Pia yumo Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu -Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Hakimu Simba wakati anatoa uamuzi huo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Faraja Nchimbi Wakili wa Serikali Mkuu, Wankyo Simon Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salim Msemo Wakili wa Serikali na Jacklin Nyantori Wakili wa Serikali huku upande wa Utete ukiwakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya na Hekima Mwasipu.

Baada ya kutoa uamuzi huo, Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo na kusema, litasikilizwa tarehe 4, 5 na 8 Novemba 2019.

Viongozi hao kwa makosa 13  yakiwamo kufanya maandamano kinyume cha sheria, kutoa maneno ya uchochezi na kufanya kusanyiko lisilohalali lililosababisha mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwelin.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!