Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Walemavu watakiwa kuwa wabunifu
Habari Mchanganyiko

Walemavu watakiwa kuwa wabunifu

Spread the love

SERIKALI imewataka viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu kuwa wabunifu katika kuibua miradi, badala ya kutegemea wafadhili. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa leo tarehe 12 Septemba 2019 bungeni na Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel (CCM).

Katika swali la nyongeza Molele alitaka kujua, serikali imejipangaje kupipatia ruzuku vyama vya watu ulemavu ili viweze kujiendesha badala ya kutumia muda mwingi kutegemea misaada.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Bumbwini, Muhammed Amour Muhammed (CUF), alitaka kujua serikali imejipanga vipi katika kuzisaidia na kuziwezesha tasisi zinazoshughulikia watu wenye ulemavu.

Akijibu swali hilo Ikupa amesema, pamoja na serikali kuwezesha vyama vya watu wenye ulemavu lakini umefika wakati ambao viongozi wa vyama hivyo kuwa wabunifu.

Amesema, iwapo viongozi wa vyama hivyo wakiwa wabunifu, itasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kujitegemea na kuondokana na utegemezi ambao unaweza kujitokea na watakuwa wameepukana na kusubiri misaada.

Aidha, amesema kwa mujibu wa sera ya taifa ya maendeleo na huduma kwa watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 na sharia na 9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu, serikali inayo majukumu mbalimbali ya kuhakikisha taasisi zinazowahudumia watu wenye ulemavu zinatoa huduma stahiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!