April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yamchoka Musiba, yamfananisha na tapeli

Cyprian Musiba

Spread the love

CYPRIAN Musiba, anayejitambulisha kuwa mwanaharakati na mtetezi wa Rais John Magufuli, amechokwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Serikali kupitia Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi imemtaka Musiba kuacha vitendo vyake vya uzushi na kudanganya wananchi kwamba, ana baraka za serikali katika uanaharakati wake.

Lugola amesema, Musiba amekuwa akifanya uanaharakati hasi unaosababisha kuchonganisha viongozi ndani ya serikali huku akijaza hofu wafanyakazi wa umma.

Mbele ya wanahabari leo tarehe 13 Septemba 2019, jijini Dodoma Lugola amemtaka Musiba kuacha kuwaaminisha kwamba, harakati zake n ahata kuchafua viongozi wa serikali zinapata Baraka kutoka serikalini.

“Aache” amesema Lugola na kuongeza “serikali haihusiki na harakati zake na akiendelea, atachukuliwa hatua.” Serikali imekuja na kuali hiyo kupindi ambacho Musiba akiwa tayari ameumiza wanasiasa na wafanyabiashara wengi kwa madai ya kumtetea Rais Magufuli.

Musiba na magazeti yake, amekuwa akilalamikiwa kuchafua viongozi wa serikali, viongozi wa wastaafu wa chama na wa upinzani akidai, anamtetea Dk. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Lugola amesema, serikali inayoongozwa na Rais Magufuli haibariki uzushi wake na kwamba, iwapo mwanaharakati huyo akiendelea na harakati hizo za kuchafua viongozi, atachukuliwa hatuakali za kisheria.

Lugola ameeleza, kitendo cha Musiba kuwaaminisha wananchi kuwa kazi ya uharakati anazozifanya, zinabarikiwa na serikali ni sawa na kufanya utapele kama walivyo mataperi wengine.

Amesema, vipo vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vinafanya kazi ya kulinda usalama wa nchi na kumsaidia mkuu wa nchi ili kuwepo kwa utulivu na siyo Musiba.

Na kwamba, Musiba amekuwa akisababisha baadhi ya watumishi kufanya kazi zao kwa hofu, kutokana na kuwaaminisha kuwa yeye anafanya kazi kwa kutumwa na Rais Magufuli kutokana na kujiita mwanaharakati huru wa kumtetea mkuu wa nchi.

Lugola amesema, wizara yake pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama, vitaendelea na uchunguzi na wakibaini kuwa anaendelea na tabia hiyo, sheria zitafuata mkondo wake.

Ameeleza kuwa, Musiba anaweza kufanya uanaharakati wake lakini usivuke mipaka na kuwaaminisha watu kuwa, yeye anafanya harakati zake kwa mkono wa serikali.

error: Content is protected !!