Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mpina: Operesheni hii marufuku
Habari Mchanganyiko

Mpina: Operesheni hii marufuku

Spread the love
OPERESHENI ya kuwaondoa wakazi wa Kijiji cha Vilimavitatu wilayani Babati, Manyara katika eneo linalodaiwa kuwa la hifadhi ya Burunge (Juhibu), imesitishwa. Anaandika Hamis Mguta…(endelea).

Wakazi hao kuanzia Julai mwaka huu, wamekuwa wakitimuliwa kwenye eneo hilo huku nyumba, mazao na nyavu zao za uvuvi vikichomwa moto.

Hatua hiyo imemsukuma Lugahaga Mpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi tarehe 6 Agosti 2019 kuagiza kusitishwa kuhamishwa kwa wakazi hao na kuacha uharibifu huo.

Luhaga amesema, Rais John Magifuli alitoa agizo la kuacha kutimua wakazi wa maeneo ya hifadhi tangu tarehe 15 Januari 2019.

Operesheni hiyo imesababisha wananchi hao kukosa mahali pa kuishi kutokana na nyumba zao kuchomwa moto, ambapo sasa wanaishi chini ya miti.

Kwenye mkutano wa hadhara wilayani humo, wananchi hao wamelalamikia hatua ya ‘kufanywa watumwa’ na serikali kwa kusumbuliwa wakidaiwa wavamizi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Elizabeth Kitundu, Mkuu wa Wilaya ya Babati ambapo wananachi wamesema, mbali na madhara hayo, akiba ya chakula chao kimechomwa moto.
“Iweje operesheni hiyo ifanyike huku kukiwa na katazo la Rais Dk. John Pombe Magufuli, la Januari 15 mwaka huu la kusitisha operesheni zote za kuwaondoa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa ni hifadhi hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo?

“Iweje operesheni ifanyike huku kukiwa na hukumu ya mahakama iliyoliondoa eneo la Kijiji cha Vilima Vitatu kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyapori Burunge (Juhibu), ambapo hukumu hiyo haikukatiwa rufaa wala kutenguliwa na mahakama?” amehoji Mpina na kuongeza;

Amesema, sheria ya haki za wanyama namba 19 ya mwaka 2010, imevunjwa katika operesheni hiyo iliyofanyika kwa wanakijiji.

“Timu ya wataalamu itakuja hapa mara moja na kuja kufanya kazi hii kwa muda wa siku saba tu, mpaka Jumapili wawasilishe taarifa yake chini ya Waziri wa Mifugo inayounda kamati hii.

“Timu hii watakuwepo Waziri wa Tamisemi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Ardhi, Waziri wa Maji, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mazingira akiwemo mwanasheria Mkuu wa Serikali. Naagiza operesheni isimame,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!