April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wizara Viwanda, Kilimo washirikiane – Mhandisi Manyanya

Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

Spread the love

WIZARA ya Viwanda na Biashara lazima ishirikiane na Wizara ya Kilimo ili kuleta tija kwa wakulima na wafugaji. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara leo tarehe 7 Agosti 2019 alipotembelea maonyesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kati katika viwanja ya Nzuguni, Dodoma.

Amesema, wakulima na wafugaji wanatakiwa kufundishwa matumizi ya teknolojia ya kisasa, waweze kufuga na kulima kisasa ili walete tija zaidi na kuongeza kipato.

“Awali wakulima walitekelezwa, lakini sasa tunasisiza zaidi makundi mbalimbali yakiwemo ya wakulima na wafugaji, yashirikishwe kufanya kazi zao kwa tija,” amesema Mhandisi Manyanya.

Amesema, wananchi wanaweza kufundishwa kutumia teknolojia rahisi katika kusindika mazao kama vile nyanya na mazao mengine, ili yasiharibike badala ya kufikiria kuwa na viwanda vikubwa ambayo siyo rahisi wajasiriamali wadogo kuvipata.

“Naona bado kuna changamoto kwa wajasirimali wadogowadogo, maeneo ya kufanyia biashara siyo rafiki kwao. Wengi wanafanyia shughuli zao juani, ni vyema wakapatiwa maeneno mazuri ili wafanye kazi zao vizuri zaidi na kuwaletea tija,” amesema Mhandisi Manyanya.

error: Content is protected !!