Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Alhaj Mwinyi: Tuvumiliane
Habari za Siasa

Alhaj Mwinyi: Tuvumiliane

Spread the love

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania kuvumiliana katika tofauti zao za kiimani. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Alhaj Mwinyi ametoa wito huo leo tarehe 31 Julai 2019, katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Misingi 15 ya Amani, kilichoandikwa jijini Dar es Salaam na Mwanazuoni wa Kiislamu, Sheikh Mohamed Iddi Mohamed.

Alhaj Mwinyi amewataka Watanzania kutodharau madhehebu ya dini “tuvumiliane katika dini zetu na madhehebu yetu, hapana shaka mtu anaamini madhehebu yake sawa sawa.

“Ndio ambayo akilala atapata usingizi, amhurumie mwingine, isiwe we mjinga hujui kitu ukitaka fuata hili langu, naye ataka usingizi vile vile,” amesema Alhaj Mwinyi na kuongeza:

“Basi tufanyeje, tuvumiliane katika madhehebu. Yako fuata vizuri namadhehebu ya mwenzio usiyadharau, dhahiri iheshimu, heshima ni mojawapo katika misingi ya dini.”

 Kwenye uzinduzi huo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewakumbusha viongozi wa dini katika tasisi mbalimbali, Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Watanzania kwa ujumla kuhamasisha wananchi kufuata misingi ya dini.

“Napenda niwakumbushe viongozi wa dini nchini hasa viongozi wa taasisi mbalimbali pamoja na wale BAKWATA viongozi wa mikoa, wilaya na maimamu wa misikiti.

“Umakini wa kiongoni una hitaji elimu uwezo na utayari. Sheikh akiwa kiongozi asiye na elimu ni vigumu kuwa makini,” amesema Sheikh Zubeir.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!