Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba: CUF iko kwenye kipindi kigumu
Habari za Siasa

Prof. Lipumba: CUF iko kwenye kipindi kigumu

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, amesema chama hicho kinapitia kipindi kigumu kwa sasa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Viongozi wa CUF mkoa wa Dar es Salaam, leo tarehe 8 Juni 2019, Prof. Lipumba amesema chama chake kimepata pigo jipya kutoka kwa vyama vya upinzani na CCM.

Ameeleza kuwa, CCM imekuwa ikiipiga vita CUF kwa kupora wabunge na madiwani wake, wakati vyama vya upinzani ikiwemo ACT-Wazalendo na Chadema vikienda kubomoa ngome za chama hicho.

“Na tuko kwenye kipindi kigumu, chama chetu kuna pigo jipya, CCM inatupiga vita, madiwani wetu wanahamishwa na wanaingia CCM, leo hii hapa hapa Dar es Salaam jimbo la Temeke ambalo ni jimbo letu la asili  na la Kinondoni,  wabunge wetu wamerubuniwa wamerudi CCM,” amesema Prof. Lipumba na kuongeza.

“Tunapigwa vita, pia na vyama vingine vya upinzani wanakwenda kujikita maeneo ya CUF hawaendi kutazama WanaCCM wawabadilishe wanajikita kwenye maeneo yetu kuwabadilisha WanaCUF waingie kwenye vyama vyao. ACT-Wazalendo, Chadema, CCM inatupiga vita kwa sababu tunasimamia haki sawa kwa watu wote.”

Prof. Lipumba amewataka viongozi wa CUF kuanzia ngazi ya chini hadi juu, kujipanga ili kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo  kuweka mikakati na sera zitakazojibu kero za wananchi kwa ajili ya kuwavutia wanawachama wake na Watanzania kwa ujumla.

Prof. Lipumba amesema ili CUF iweze kushindana na vyama vingine vya siasa, inatakiwa iweke misingi thabiti itakayoiwezesha kushinda uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020.

“Viongozi wa Dar es Salaam tuna kazi ya ziada ya kujipanga katika taratibu nzima ya kuweka wagombea katika kila mtaa wa jiji la Dar, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaokuja, kazi yenu kama viongozi ni kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujua kwanza kero za wananchi,” amesema Prof. Lipumba na kuongeza.

“Mjipange namna ya kuboresha mazingira ili kuondokana na matatizo, lazima tujipange kujibu kero za wananchi, wafanyabiashara ndogo ndogo, mamantile. Mazingira ya biasharakwa ujumla sio rafiki matokeo yake hali inakuwa ngumu.”

Aidha, Prof. Lipumba ameweka bayana kwamba ifikapo tarehe 22 Juni mwaka huu, CUF itatangaza sera zake mpya,  ambazo zinakidhi mahitaji ya Watanzania.

“Wekeni kwenye kalenda tarehe 22 CUF mpya inakuja na sera muafaka za kukidhi mahitaji ya watanzania.  Tunakuja na sera muafaka za kudai demokrasia, haki sawa kwa wote , sera za kuleta furaha kwa Watanzania. Asie na mwana aeleke jiwe, zile sera za ngangali kinoma zinakuja,” amesema Prof. Lipumba.

Kauli hiyo ya Prof. Lipumba kwamba CUF ina pigo jipya imekuja ikiwa ni miezi miwili na siku kadhaa kupita, tangu kumalizika kwa mgogoro wa kiuongozi uliokuwemo ndani ya chama hicho, kufuatia aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad kuhamia chama cha ACT-Wazalendo na kundi la wafuasi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!