Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Familia yarejesha ‘uhai’ wa Kapteni Komba
Habari Mchanganyiko

Familia yarejesha ‘uhai’ wa Kapteni Komba

Spread the love

FAMILIA ya aliyekuwa gwiji wa sanaa nchini, Kapteni Jonh Komba, inatarajia kuzindua taasisi ya kumbukumbu ya kuenzi sanaa yake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Sambamba na kuanzisha bendi ya muziki itakayoimba sauti ya Kapteni Komba, familia hiyo imeipa taasisi hiyo jina la The Capten Komba Arts Memorial Foundation.

Kapteni Komba ambaye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, alifariki siku ya Jumamosi tarehe 28 Februari 2015 katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya familia na taasisi hiyo, Salome Komba, mjane wa Kapteni Komba ambaye pia ndio katibu wa taasisi hiyo amesema, uzinduzi wa taasisi hiyo utakwenda sambamba za uanzishwaji wa bendi ya muziki itakayoenzi sanaa ya Kapteni Komba.

Taasisi hiyo itazinduliwa tarehe 6 Julai 2019 katika ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa, Kijitonyama, Dar es Salaam.

”Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Bashiru Ali na kuhudhuriwa na wabunge mbalimbali pia viongozi wa serikali pamoja na wasanii,” amesema Mama Solome.

Amesema kuwa, taasisi hiyo imejenga makumbusho ya kumuenzi Kapteni Komba ambapo ujenzi wake ulizinduliwa na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, terehe 28 Februari 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!