Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Kisangi: Uhaba shule za walemavu ni kikwazo
Habari za Siasa

Mbunge Kisangi: Uhaba shule za walemavu ni kikwazo

Spread the love

MBUNGE Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Mariam Kisangi ameishauri serikali kuongeza idadi ya shule za watoto wenye mahitaji maalumu, akisema wengi wao wanakosa elimu kutokana na changamoto ya uhaba wa shule hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 31 Mei 2019 Mariamu amesema kume kuwepo na ongezeko la watoto wenye mahitaji maalum, na kwamba shule zilizopo hazina uwezo wa kubeba idadi hiyo.

“Kumekuwa na ongezeko la watoto wenye mahitaji maalum, kwa kuwa shule maalum zilizopo zinakuwa hazitoshelezi mahitaji, serikali haioni sababu ya kuongeza vitengo vya watoto wenye mahitaji maalum ili na wao waweze kupata elimu kwenye maeneo wanayotoka?” amehoji Mariam.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitara amesema serikali imekwisha toa agizo kwa halmashauri nchini kuhakikisha kwamba wanajenga  miundombinu rafiki kwa watoto wenye uhitaji kwenye shule zilizopo nchini.

“Baada ya kuona unapotenga shule maalum unakuwa unawatenga, sasa imekuja elimu jumuishi, na tumetoa agizo kwenye ujenzi wa miundombinu iweke miundombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, na wanafunzi wawaone kuwa hao ni wenzao, na tunaongeza nguvu na ombi lako tutalifanyia kazi,” amejibu Waitara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!