Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mambo ya Nje yaomba Bil 166
Habari za Siasa

Mambo ya Nje yaomba Bil 166

Prof. Palamagamba Kabudi
Spread the love

WIZARA ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeomba bajeti ya ya Sh. 166.92 bilioni kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akiwasilisha maombi hayo bungeni leo tarehe 30 Mei 2019 Prof. Palamagamba Kabudi amesema, fedha hizo ni kwa ajili ya mambo mbalimbali ya wizara hiyo ikiwemo mishahara, Mpango wa Kujitathimini Kiutawala Bora Tanzania (APRM), fedha kwa ajili ya maendeleo pamoja na matumizi mengine.

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo amesema, katika Sh166.92bilioni mishahara ni Sh 10.2 bilioni ambapo Sh. 2.5 bilioni zitatumika mishahara ya watumishi wa Chuo cha Diplomasia na Sh 4 Bil kwa ajili ya maendeleo.

Katika fedha za matumizi mengineyo amsema, Sh 948 milioni zitatumika kwa ajili ya APRM, Sh 158.27 milioni za  Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika, Sh1.23 bilioni ni kwa ajili ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na Sh 1 bilioni ni kwa matumizi mengine katika Chuo cha Diplomasia.

Waziri huyo amelieleza Bunge kwamba, Sh 1 bilioni ni kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya ubalozi wa Tanzania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Sh 100 milioni zitatumika kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo  ubalozi wa Tanzania Khartoum, Sudan.

Pia Sh 800 milioni zitatumika katika kukarabati wa majengo ya makazi ya watumishi wa ubalozi wa Tanzania Lusaka nchini Zambia ambapo Sh 450 milioni zitatumika kwa kuweka miundombinu ya umeme katika jengo la wizara lililopo Dar es Salaam.

Pia amesema, jumla ya Sh 300 milioni zitatumika katika ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya wizara iliyopo Mtumba jijini Dodoma na Sh150 milioni ni kwa ajili ya ukarabati wa makazi ya Balozi wa Tanzania Ottawa, Canada pia jumla ya Sh200 milioni zitatumika kwenye ujenzi wa uzio wa kiwanja cha Serikali kilichopo ubalozi wa Tanzania Nairobi, Kenya ambapo Sh 1 bilioni zitatumika kwenye upanuzi wa miundombinu ya Chuo cha Diplomasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

error: Content is protected !!