April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mgogoro wa bei Pamba wapatiwa ufumbuzi

Spread the love

MGOGORO wa bei ya zao la pamba ulioukuwepo baina ya wakulima na wanunuzi umemalizwa na sasa zao hilo litaendelea kununuliwa kwa bei elekezi ya Sh. 1, 200 kwa kilo. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mgogoro huo umemalizwa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kukutana na makundi ya wanunuzi na wakulima jijini hapa ili kujadili kwa pamoja kuhusu bei ya ununuzi wa pamba hiyo.

Waziri mkuu, alisema katika kukithamini kilimo cha pamba, Serikali iliitisha vikao vingi tangu mwaka jana kwa ajili ya kuimarisha zao hilo na kwamba dhamira yake ni kuhakikisha kilimo cha pamba kinamnufaisha mkulima.

Waziri Majaliwa alisema katika msimu uliopita ulileta mafanikio makubwa kwa kuzalisha zao hilo kutoka tani 222,000 hadi kufikia karibu tani 450,000 kwa msimu wa mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu Majaliwa, aliwahakikishia wakulima kuwa zao la pamba ni kati ya mazao muhimu na kwamba pamba yote iliyolimwa msimu huu itanunuliwa yote.

Pia amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yao kuangalia utaratibu mzuri wa kuwasaidia wanunuzi ili kuhakikisha pamba yote inayonunuliwa kutoka kwa mkulima inawafikia salama.

“Nendeni mkaweke mifumo ya fedha iliyopo kama iko sawa ili wakulima wetu waweze kulipwa fedha zao kupitia benki nah ii itasaidia zaidi wakulima.

“Lengo letu kama serikali kama serikali ni kuhakikisha mwenendo wa manunuzi unakwenda vizuri,” alisema na kuwahakikishia wanunuzi kuwa biashara yao itasimamiwa vizuri,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Katika hatua nyingine, waziri mkuu, alihimiza kuendelea kutunzwa kwa ubora wa pamba na kuweka mikakati ili kuimarisha zao la pamba.

Hata hivyo, Waziri Majaliwa, mikakati hiyo ya uboreshaji wa zao la pamba itakwenda pamoja na uimarishaji wa utoaji wa elimu kwa wakulima wote kuhusu ubora wa zao la pamba.

error: Content is protected !!