Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kutekwa Mo: Dereva teksi asomewa mashtaka matatu
Habari MchanganyikoTangulizi

Kutekwa Mo: Dereva teksi asomewa mashtaka matatu

Spread the love

MOUSA Twaleb ambaye ni dereva teksi, leo tarehe 28 Mei 2019, amepandisha katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akituhumiwa kwa makosa matatu likiwemo la kumteka Mohammed Dewj (Mo). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Shtaka la kwanza, mtuhumiwa anadaiwa kuhusika kwenye mtandoa wa kihalifu ambapo anadaiwa kati ya tarehe 1 Mei na 10 Oktoba 2018 maeno ya Mbezi Beach, Dar es Salaam na Johnsburg Afrika Kusini alitoa msaada kwa wenzake ambapo hawapo mahakamani kutenda vitendo vya jinai kwa nia ya kujipatia fedha.

Shtaka la pili ni kutekanyara, inadaiwa tarehe 11 Oktoba 2018, kwenye Hotel ya Collusium Hotel Masaki, Kinondoni mtuhumiwa na wengine ambao hawapo mahakamani walimteke nyara Mo na kumhifadhi kwa siri.

Shtaka la mwisho ni utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa mtuhumiwa akiwa eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam tarehe 10 Julai alijipatia Sh.8 Milioni kwa kujua kuwa pesa hizo ni mazalia ya uhalifu alizozipata kutoka kwenye genge la kihalifu.

Hata hivyo, Wakili Kadushi aliieleza mahakama kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika sehemu kubwa na kwa kuwa, kesi hiyo ni uhujumu uchumi kuna taratibu zake.

Twaleb (46) amefikishwa mahakamani hapo leo saa mbili asubuhi na kusomewa mashitaka yake mbele ya Huruma Shaidi, Hakimu Mkazi Mkuu.

Mo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Timu ya Soka ya Simba (SCC), alitekwa tarehe 11 Oktoba 2018 alfajir wakati akitoka kufanya mazoezi katika Hoteli ya Colosseum iliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, alipatikana tarehe 20 Oktoba 2019 akiwa ametelekezwa kwenye Viwanja vya Gymkhana ambapo watu 12 walikamatwa wakihusishwa na tukio la kutekwa kwake.

Ukimya wa Jeshi la Polisi baada ya kupatikana kwa Mo ulimkera Rais John Magufuli ambapo tarehe 4 Machi 2019 alisema, ukimwa huo uliacha maswali mengi kwa wananchi.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo wakati akiwaapisha mawaziri Prof. Palamagamba Kabudi na Balozi Augustino Mahige Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Mtu aliyetekwa, alikutwa Gymkhana lakini watu wanajiuliza mmmh aliendaje pale, lakini alipowekwa pale na bundeki zikaachwa pale, unajiuliza huyu mtekaji aliamua kuziachaje? Angekutana na polisi wanaomtafuta njiani?” alihoji Rais Magufuli.

Baada ya Mo kutekwa, familia yake iliahidi kutoa donge la Sh. 1 Bil kwa yeyote angefanikisha kupatikana kwake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

error: Content is protected !!