Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri: ‘Tumepigwa’ sana
Habari za Siasa

Waziri: ‘Tumepigwa’ sana

Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria
Spread the love

MIKATABA mingi inayoingiwa na wizara, taasisi za umma na wadau mbalimbali nchini, imekuwa na udanganyifu mkubwa na kusababisha taifa kupata hasara. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 28 Mei 2019 bungeni jijini Dodoma na Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbena aliyehoji kiwango cha hasara kilichoingia serikali kutokana na kusitisha baadhi ya mikataba.

Balozi Mahiga amesema, kufuatia mikataba mingi kuwa na udanganyifu unaoliletea taifa hasara, serikali iko katika zoezi la kupitia mikataba yote iliyoingiwa na wizara pamoja na taasisi za umma na wadau mbalimbali nchini, ili kusahihisha upungufu uliyokuwemo.

“Ni lazima tuangalie kwa umakini, mikataba mingi ina udanganyifu, tunapoisaini tunaweza kudanganywa, ndio maana wizara yangu imeona kuna umuhimu wa kufanya marekebisho na kusahihisha mapungufu yote ya wizara zote na taasisi zote zoezi linaendelea,” amesema Balozi Mahiga.

Kuhusu swali la Mbena, Balozi Mahiga amejibu kuwa, kwa sasa serikali haiwezi kutoa takwimu za idadi ya mikataba iliyositishwa na kesi zilizofunguliwa dhidi yake hadi pale idara iliyoundwa ya kusimamia mikataba itakapokamilisha ufuatiliaji wa mikataba hiyo.

Balozi Mahiga amesema, idara hiyo iliyoko chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), inapitia mikataba yote iliyositishwa, inayotarajiwa kusitishwa na inayotakiwa kufanyiwa marekebisho, na kwamba zoezi hilo likikamilika serikali itatoa takwimu sahihi kuhusu kesi hizo.

“Serikali kupitia idhini ya Rais John Magufuli, imerekebisha majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo imeanzisha idara ya kusimamia utekelezwaji wa mikataba yote.

“Hii itasaidia kutoa takwimu sahihi ya mikataba iliyositishwa, inayotarajiwa kusitishwa na inayotakiwa kufanyiwa marekebebisho na gharama zake,” amesema Balozi Mahiga.

Amesema, ofisi hiyo inaendelea na kazi ya utambuzi wa mashauri yote dhidi ya ya serikali, kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi na mashauri yaliyofunguliwa kutokana na ukatishwaji wa mikataba.

Aidha, Balozi Mahiga amesema, serikali inaendelea kufuatilia kwa ukaribu matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, hasa baadhi ya watu kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana na wananchi kuchukua sheria mkononi kuwa watu wanaotuhumiwa kufanya makosa mbalimbali.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Malindi, Ally Saleh aliyehoji ukimya wa serikali kuhusu matokeo ya uchunguzi wa matukio hayo pamoja na wanaohusika kutochukuliwa hatua stahiki.

 “Matukio ambayo umeyataja na ambayo yametokea yanajulikana serikalini na vyombo husika hasa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama vimekuwa vikifuatilia matukio hayo.

“Mara nyingi tunapata taarifa na majibu yanaridhisha lakini kazi ya upelelezi na ya kufuatilia vitendo hivyo inaweza ikachukua muda na serikali imekubali kuchukua jukumu hilo,” amesema Balozi Mhaiga.

Amesema, vyombo vya ulinzi na usalama vitakapokamilisha upelelezi wa matukio hayo serikali itatoa taarifa sahihi kwa wananchi na jumuiya za kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!