Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Masele ashusha mashambulizi
Habari za Siasa

Masele ashusha mashambulizi

Stephen Masele, Makamu Rais wa Bunge la Afrika Mashariki (PAP)
Spread the love

STEPHEN Masele, Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM) amesema, hana tabia ya kueleza jambo kwa namna anavyopenda mtu isipokuwa kwa uhalisia wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“…kama unafikiri nitakwenda kukuambia kile unachotaka kusikia, siko hivyo kwasababu nitakwenda kukueleza kile ninachokiona,” ameandika Masele kwenye ukurasa wake wa twitter leo tarehe 16 Mei 2019.

Ameandika maneno hayo muda mfupi baada ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kulieleza Bunge taarifa ya kusimamisha uwakilishi wake kwenye Bunge la Afrika (PAP) leo.

Mbunge huyo ameeleza kuwa, hawezi kushughulika na vitu vidogo kwa kuwa, yeye ni msomi na amelelewa katika malezi ya maadili na nidhamu.

Tayari Spika Ndugai ameagiza Masele kwenye kuhudhuria kikao cha Kamati ya Maadili ili athibitishe tuhuma zake ambazo hakuzitaja.

Spika Ndugai amemtuhumu Masele kufanya utovu wa nidhamu na kugonganisha mihimili miwili ya nchini (Bunge na Serikali).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Masele ameandika kuwa, wazazi wake wamemlea vyema katika kusimamia thamani na heshima ya jamii.

Pia ameandika kuwa, ataendelea kueleza mambo anayoyaona hata kama kuna mtu hataki kusikia huku akisisitiza kuwa, PAP ina itifaki na kanuni zake.

Akiwa bungeni Spika Ndugai amesema, Jumatatu ya tarehe 13 Mei 2019 alimuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Masele katika bunge lake, hadi pale Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Spika Ndugai amesema, Masele ameitwa kuhojiwa kutokana na kutoridhidhwa na mwenendo wake, lakini amekaidai kwamba, anafanya mambo ya hatari.

“Kwa mtazamo yetu amekuwa akifanya mambo ya hatari kubwa, ikiwemo kugonganisha mhimili, anapeleka kwenye mhimili wa serikali juu kabisa maneno mengi ya uongo, ushahidi hupo, na kulidhalilisha bunge,” amesema Spika Ndugai.

Akitoa taarifa hiyo Ndugai amesema kuwa, anazo taarifa mbili muhimu ambapo alisema kuwa alitaka kuliambia bunge kuwa taarifa hizo ni pamoja na hatua zilizofikiwwa katika ukaguzi wa hesabu za ofisi ya taifa ya ukaguzi (CAG).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!