Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai alianzisha upya kwa Prof. Assad
Habari za SiasaTangulizi

Spika Ndugai alianzisha upya kwa Prof. Assad

Prof. Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali. Picha ndogo Job Ndugai, Spika wa Bunge
Spread the love

MNYUKANO kati ya Job Ndugai, Spika wa Bunge na Profesa Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), bado unaendelea. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Spika Ndugai amelieleza Bunge leo tarehe 16 Mei 2019 kwamba, Bunge limepokea ripoti ya ukaguzi wa hesabu katika ofisi ya CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2018.

“Kwa mujibu wa kifungu 46, kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya ukaguzi wa Umma sheria namba 11 ya mwaka 2008, hesabu za CAG yaani za ofisi ya taifa ya ukaguzi zinapaswa kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka.

“Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ina jukumu la kuteua mkaguzi wa kukagua hesabu za ofisi hiyo. Kwa maneno rahisi, Bunge ndio tunatafuta mkaguzi wa nje ambaye ndiye anayekagua hesabu za CAG,” amesema Spika Ndugai na kuongeza;

“Kwa hiyo, ukaguzi ulishafanyika huko nyuma na Kampuni ya Mkaguzi inaitwa EKI MANGESHO KAMPANI…, imefanya kazi hiyo ya ukaguzi na imetuletea taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za ofisi hiyo.”

Prof. Assad na Spika Ndugai wameingia kwenye msuguano kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, baada ya Pro. Assad kusema ‘Bunge  ni dhaifu’ alipokuwa nje ya nchi. Tayari Bunge limetangaza azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad.

Akizungumzia taarifa hiyo Spika Ndugai amewaambia wabunge kuwa, ameona afanye hivyo na kwamba, pamoja na CAG kuweka mezani hesabu za taasisi zingine, taasisi hiyo hesabu zake huwa haziweki mezani.

“Nimeona niwajulisheni ili muweze kufahamu katika hesabu zilizowekwa mezani wakati ule, hesabu za ofisi ya CAG mwenyewe huwa haziwekwi mezani, utaratibu wake ni huu ninaoeleza.

“Kunakuwa na mkaguzi kutoka nje anakagua. Nawataarifu sasa bungeni kuwa, nimeishapokea taarifa hiyo na nimeishaipitia, kuna mambo lakini utaratibu ni kwamba, tunapeleka kwenye kamati ya PAC (Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali),” amesema.

Spika Ndugai amesema, kwa kwa kuzingatia sheria ya ukaguzi, ripoti hiyo hiyo anaipeleka PAC ili ipitie na kuichambua.

“Mara itakapomaliza, itawasilisha uchambuzi huo kwangu na mambo mengine yatakayofuatia ni yale ambayo yatakuwa ya wakati huo, katika masuala ya ukaguzi, hakuna anayebaki na hakuna anayejikagua mwenyewe, kila watu wanaangalia wenzao,” amesema Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!