Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Anayedaiwa kutumia jina la Katibu Mkuu CCM kutapeli akamatwa
Habari Mchanganyiko

Anayedaiwa kutumia jina la Katibu Mkuu CCM kutapeli akamatwa

Spread the love

JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Wilfred Welandumi kwa madai ya kutumia jina la Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya utapeli. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 5 Aprili 2019, SACP Lazoro Mambosasa, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema, jeshi hilo limemwanika Welandumi (40) ili kuwapa wananchi tahadhari.

Kamanda Mambosasa amesema, Welandumi ni mkazi wa Yombo, Dar es Salaam.

“Mtuhumiwa huyo amekuwa akiwapigia simu baadhi ya wabunge wa chama tawala na kuwaomba fedha kwa kujifanya yeye ni Dk. Bashiru na hatimaye kufanikiwa kutapeli fedha kiasi cha Tsh. 370,000,” amesema.

Na kwamba, mtuhumiwa huyo hakutumia jina la Dk Bashiru pekee yake bali hata jina Prof. Makame Mbarawa ambaye sasa ni Waziri wa Maji.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!