Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CUF: Sijali, nakwenda ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge CUF: Sijali, nakwenda ACT-Wazalendo

Spread the love

YUSUF Salim Hussein, Mbunge Jimbo la Chambani visiwani Zanzibar amesema, hahofii kufukuzwa na kwamba, hayupo tayari kubaki Chama cha Wananchi (CUF).Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hussein ametoa kauli hiyo licha ya kuwepo kwa wito uliotolewa na Halifa Suleiman Halifa, Katibu Mkuu wa CUF, kwamba wabunge wa chama hicho ‘waliowatusi’ viongozi wao waende kuungama ili wasifukuzwe.

Mbunge huyo amesema kuwa, nakwenda kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo kwa kuwa, hana sababu ya kubaki CUF.

Na kwamba, Chama cha CUF kimepoteza uhai kwani, kinachofanya kipumue kwa miezi 15 kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao ni ‘viruzuku’ tu.

“CUF imekufa, haipo. Wewe unaiona CUF? Itadumu labda kwa sababu ya hivi ‘vi-ruzuku’ kwa huu mwaka mmoja na nusu uliobakia wa uhai wa Bunge. Baada ya hapo, CUF haipo,” amesema mbunge huyo alipozungumza na gazeti moja la kila siku hapa nchini.

Amesema, Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho ameondoka na wanachama wake jambo ambalo limeiathiri CUF kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza kwenye mahojiano hayo Hussein amesema, Maalim Seif ametoka na watu wote waliosimama naye wametoka.

Na kwamba, kwa kuwa CUF hakina pumzi tena, anasubiri muda wa kwenda kujiunga na ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na kwamba, ndio mbadala wa CUF.

“”Msimamo wangu unaeleweka na upo wazi kabisa. Mimi ni mbunge wa CUF kwa sasa lakini sibaki CUF, nakwenda zangu ACT-Wazalendo.

“Kama nitamaliza kipindi hiki sawa, na kama sintomaliza sawa lakini nakwenda ACT-Wazalendo.

Wala sitafuni maneno katika hilo, nasisitiza nakwenda ACT-Wazalendo, huko ndiko kuliko ‘ShushaTangaPandishaTanga Safari iendelee’.

Hussein amasema, kwa sasa anaendelea kubaki CUF kwa kuwa, wananchi wamemchagua kupitia chama hicho ili kuwakilisha kero zao bungeni na si vinginevyo.

“Mimi ni mbunge kwa sasa kwa kuwa wananchi wamenichagua, lakini nikiambiwa leo ondoka, basi naondoka, wala sina tatizo, kabisa!” amesema.

Amesema kwamba, mara kadhaa CUF ilikuwa ikipiga kelele kwamba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wamekuwa wakipanga kuua chama chao.

“Hili tumesema sana, sasa kama chama ni jina, sawa lakini CUF bali ni wanachama, ndio maana wanachama wanaondoka CUF. Chama ni watu sio jina,” amesema na kuhoji;

“Maalim katoka na watu wote wametoka. Sasa wao wanahangaika tu, si walitaka chama, wameachiwa chama, sasa kwanini wanababaika?”

Mbunge huyo wa Chambani amesema, kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kama uchaguzi utakuwa huru na haki, ACT-Wazalendo inaweza kupata wabunge zaidi ya 30 visiwani Zanzibar.

“Si kwa ACT-Wazalendo, chama chochote tutakachoamua kwenda sisi, si wamesema wanataka kukifuta chama cha ACT, wakifute,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!