Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yatangaza fursa za Utalii kwa wawekezaji
Habari Mchanganyiko

Tanzania yatangaza fursa za Utalii kwa wawekezaji

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda akiwa na timu ya wawekezaji wakiangalia fursa za uwekezaji nchini
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Professa. Adolf  Mkenda, amesema serikali imeanza mipango na mikakati itakayosaidia wizara hiyo kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kuimarisha mfumo wa kielektroniki wa usajili wa wakala wa biashara za utalii. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Amesema kutokana na umuhimu wa sekta hiyo, tayari wizara hiyo imevitangaza vivutio vilivyopo nchini, kupitia masoko ya utalii wa kimataifa pamoja na kuupa sura mpya utambulisho wa Tanzania katika sekta ya Utalii.

 Professa Mkenda ametoa kauli hiyo jijini Mwanza, wakati alipoongoza timu ya wawekezaji kutembelea Mapori ya Akiba ya Biharamuro, Burigi na Kimisi, kuangalia fursa za uwekezaji.

Alisema kuwa mipango yote inayofanyika na wizara yake inalenga kuongeza na kuchochea ukuaji wa utalii nchini kutokana Tanzania kubarikiwa vivutio vingi.

Sanjari na hayo, Professa Mkenda amesema wizara hiyo imeanza kushirikiana na Shirika la ndege Tanzania (ATCL), kuhamasisha na kuwezesha watalii wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali kufika kwa urahisi hapa nchini.

Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kwa kasi  kubwa ndani na nje ya nchi fursa za uwekezaji,  kwenye maeneo ya vivutio vilivyopo nchini katika kanda zote za Utalii, ikiweka mkazo zaidi kwenye Utalii wa mikutano, fukwe na meli, utalii wa kihistoria na kiutamaduni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!