Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Watoto 5,500 watazaliwa 2019, UNICEF wajipanga kwa usalama wao
AfyaHabari Mchanganyiko

Watoto 5,500 watazaliwa 2019, UNICEF wajipanga kwa usalama wao

Spread the love

SHIRIKA la Wototo Duniani (UNICEF) limeeleza kuwa siku ya mwaka mpya kutazaliwa watoto 395,072 ambapo nchini Tanzania watazaliwa watoto 5,500 ambao ni sawa na asilimia 1.4 ya watoto watakaozaliwa siku hiyo dunia mzima. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hata hivyo UNICEF imeweka wazi kuwa nchini Tanzania vifo vya watoto wa mwezi mmoja hadi mwaka mmoja vimepungua kwa asilimia 40 tangu mwaka 2005 kutokana uboreshwaji wa miundombinu ya afya ingawa bado vifo hivyo vinaendelea ambapo watoto wengi hufa mwezi mmoja baada kuzaliwa kutokana na ugonjwa wa malaria, kuhara na ammonia.

Unicef inaeleza kuwa watoto zaidi ya 300 hufa kila siku kutokana na kushambuliwa kwa magonjwa hayo yanayofanya idadi ya vifo vya aina hiyo vinavyotokea mwezi wa kwanza baada ya kuzaliwa kufikia asiliamia 40.

Kupitia taarifa ya Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Said Maniza Zaman ameeleza kuwa mwezi Novemba mwaka 2018 Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF ilianziasha kampeni ya jiongeze iliyolenga kuokoa vifo vya watoto.

“Hatutachoka mpaka watoto watakapokuwa wakizaliwa salama, mwaka mpya tutapambana kuhakikisha tunawasaidia kupata haki yao ya kila mmoja kuwa salama, tutaokoa maisha ya watoto milioni kwa kuwa na vifaa tiba bora na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya kwenye zahanati,” amesema Zaman.

Zaman amesema kuwa UNICEF inaelekeza nguvu ya kumaliza kabisa vifo vya mama na watoto kwa kulenga mwaka wa 2019 kwa dunia mzima itaendesha kampeni za kuokoa maisha yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!