Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Mchungaji: Mkristo kukwepa kodi ni dhambi kubwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Mchungaji: Mkristo kukwepa kodi ni dhambi kubwa

Mashine ya EFD
Spread the love

MCHUNGAJI Kiongozi wa kamisa la Evangelisim Assembless Of God Tanzania (EAGT) Ipagala, Evanci Chande amewaonya wakristo wafanyabiashara ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi ya serikali. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mchugaji Lucas alitoa onyo hilo katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu,iliyofanyka kanisani hapo kwa lengo la kuwaombea waumini wa kanisa hilo waweze kufanikiwa katika shughuri zao za Kiroho na kimwili kwa kipindi cha mwka 2019.

Katika ibada hiyo ambayo iliambatana na shukrani mbalimbali za kumshukuru Mungu kuvuka salama mwaka uliopita na kuingia mwaka huu mchungaji huyo alisema kwamba ili kuweza kuendelea vyema ni lazima kufanya kazi ambazo zina utukufu mbele za Mungu.

Hata hivyo alisema kuwa ni aibu kwa mkristo ambaye ni mcha Mungu na ni mfanyabiashara ambaye anakwepa kodi ya serikali kwani kwa kufanya hivyo ni kuliibia taifa na kusababisha kushuka kwa maendeleo ya nchi.

“Nawatangazia Wakristo wote nchini pamoja na waumini wa kanisa hili ni dhambi kubwa kwa mfanyabiashara kukwepa kodi ya serikali na ijulikane wazi kuwa kodi ni mpango wa Mungu kabisa kwani hata enzi za Yesu mafarisayo walimuuliza Yesu swali la mtego juu ya kodi.

“Lakini kwa kuwa kodi ni jambo la Kimungu Yesu aliweza kuwajibu kwa kusema “Iko wapi hiyo sarafu baada ya kumuonesha aliwauliza hii sarafu ina sura ya nani nao wakamjibu kuwa ina sura ya Kaisali akawajibu cha Kaisali mpe Kaisali na cha Mungu mpe Mungu” kwa maana hiyo kodi ni agizo kutoka kwa Mung,” alisema Mchungaji Chande.

Katika hatua nyingine mchungaji huyo amewataka waumini wa kanisa hilo ambao wapo maofisini ambao wanazo ajira mbalibali kuhakikisha wanafanya kazi kwa misingi ya uaminifu na kujituma pamoja na kuhakikisha maendeleo ya taifa yanasonga mbele.

Katika mahubiri yake Mchungaji Chande alisema mwaka 2019 ni mwaka wa mabadiliko makubwa sambamba na kuhakikisha amani ya nchi inatunzwa kwa gharama yoyote huku akiwasihi wanafunzi wa vyuo vikuu kujikita zaidi katika masomo yao na kuepukana na vishawishi vya kuanzisha migomo.

Kuhusu suala la kilimo Mchungaji Chande aliwataka wakulima kulima kilimo cha kisasa kwa lengo la kupata mazao mengi ambayo wataweza kuuza katika soko la ndani na nje kwa faida yao na taifa kwa ujumla.

“Nyie wakulima limeni kilimo cha kisasa na chenye tija ili muweze kuuza katika masoko ya ndani nay a nje na kutunzachakula cha kutosha watumieni wataalamu wa kilimo na wala msiwaze kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo latafuta dawa kwa lengo la kupata mazao mengi.

“Zingatia mambo muhimu wakati wa kulima,tumia wataalamu, tumia mbegu bora na anza kuandaa na kupanda kwa muda mwafaka ili kuweza kupata mazao ambayo yatakuwa na tija zaidi,” alisema Chande.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

error: Content is protected !!