Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Matukio ya michezo/sanaa yaliyotikisa 2018
MichezoTangulizi

Matukio ya michezo/sanaa yaliyotikisa 2018

Rais John Magufuli akimkabidhi Kombel la Ubingwa wa LIgi Kuu Bara, nahodha wa Simba, John Bocco
Spread the love

MWAKA 2018 unafikia tamati, katika miezi 12 inayokamilika leo wapo watu wanauaga mwaka kwa machungu yasiyosahaulika kwenye maisha yao milele lakini wapo wanaouona kuwa, ni mwaka wa neema kwao. Anaandika Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Katika michezo na sanaa, ipo mitikisiko mikubwa imewakumba viongozi, timu zao, vyama vinavyosimamia michezo hiyo na hata sanaa hivyo kusababisha kuibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii. Haya yafuatayo ni baadhi ya matukio ya kimichezo yaliyoweka historia nchini;-

Rais Magufuli kuwakabidhi Simba Ubingwa wa Ligi Kuu 2017/18

Mei 19, kwa mara ya kwanza tulishuhudia Rais wa Jamhuru ya Muungani wa Tanzania John Magufuli kushiriki kushiriki kwenye tukio la kimichezo toka alipoingia madarakani 2015, ambapo alifanjikiwa kuwakabidhi klabu ya Simba ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mcheoz uliowakutanisha Simba na Kagera Sugar.

Katika tukio hilo Rais Magufuli alizungumza na Familia ya wana michezo na kuonesha masikitiko yake namna ambavyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF jinsi ambavyo linavyoendesha mpira wan chi hii kutokana na kuwa na matumizi mabaya ya fedha kiasi kilichopelekea kukosa baadhi ya Fedha amabzo zilikuwa zinatolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA.

Hata katika siku hiyo hiyo Rais Magufuli alipokea kombe kutoka kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambao walitwaa ubingwa wa Challenge nchini Burundi na kusisitiza kuwa timu za Tanzania ziweze kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa ili kuleta heshima nchini.

Bondia kutoka Tanzania kushinda pambano Uingereza

8 Septemba, 2018 bondia kutoka Tanzania Hassan Mwakinyo mwenye umri wa miaka 23 alifanikiwa kumtwanga bondia kutoka Uingereza Sam Egginton kwa KO kwenye raundi ya nne katika pambano la utangulizi kwenye mchezo baina ya Amir Khan na Samuel Vergasn uliofanyika Birmingham kwenye kitongoji cha West Midlands.

Kufariki kwa Msanii wa vichekesho Mzee Majuto

Ilikuwa Agosti 9,2018 ambapo Tanzania tulimpoteza Msanii mkongwe wa Vichekesho Amri Athuman maarufu kama ‘King Majuto’ ambaye alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Majuto alilazwa hospitalini hapo toka Julai 31, baada ya kutoka nchini India alipokua ameenda kwa ajiri ya matibabu ya Nyonga mara baada ya Serikali kwa kushirikiana na Wananchi kuchanga pesa za matibabu hayo.

Mkongwe huyo alitangaza kustaafu kuigiza mara baada ya kuanza kuumwa, atakumbukwa kwa kazi zake nyingi za kuchekesha ambazo alizifanya kwa uhodari mkubwa na kuwavutiwa mashabiki wengi na kujizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu.

Simba kufuzu kwenye hatua ya makundi katika michuano ya klabu bingwa

Baada ya miaka 15 hatimaye klabu ya Simba imefanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani afrika kwa mwaka huu baada ya kuiondoa klabu ya Nkana Fc kutoka Zambia kwa jumla ya mabao 4-3.

Simba ambao wamepangwa katika kundi D kwenye michuano hiyo sambamba na klabu za Al Ahly, JS Saoura na As Vital kama wakifanikiwa kuvuka hapo wataingia katika hatua ya robo fainali.

Mahakama yamrejesha Wambura TFF

Baada ya kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kufungiwa Michael Wambura ambaye ni makamu Rais wa TFF kushiriki mambo ya mpira wa miguu katika maisha yake yote.

Hivi karibuni Mahakama kuu ya Dar es Salaam kupitia Jaji Dk Benhajji Masoud ilitengua maamuzi ya kamati hiyo na kumrejesha Wambura madarakani licha ya TFF kupitia katibu mkuu Wilfred Kidau kukataa rufaa juu ya hukumu hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!