Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chungu na tamu ya siasa 2018
Habari za SiasaTangulizi

Chungu na tamu ya siasa 2018

Maandamo ya wafuasi wa Chadema
Spread the love

TAMATI ya mwaka 2018 inakaribia, yapo yaliyofurahisha na kuchukiza. mwaka inakwisha huku taifa likibeba matukio mengi. miongozini mwayo yanahuzunisha na hata kuumiza mtu mmoja mmoja ama taifa kwa ujumla, lakini pia yapo yanayotoa faraja kwa taifa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Miongoni mwayo ni pamoja na tarehe 5 Julai Mwaka 2018 Halima Mdee Mbunge wa Kawe alitiwa mbaroni na jeshi la Polisi kisha alifikishwa mahakamani terehe 10 Julai kwa kosa la kutoa lugha ya kashfa kwa Rais John Magufuli kwa kusema kuwa “Rais magufuli anaongea hovyohovyo anatakiwa afungwe break’ kwenye mkutano wake na vyombo vya habari.

Siku ya tarehe 20 Febriari viongozi saba waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliitwa kwenye kituo kikuu cha kati cha Polis kwa ajili ya mahojiano ya jeshi la Polisi na viongozi hao kuhusu maandamano yao ya ijuma Februari 17 mwaka 2018 na kuhusu mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Akwilana Akwili aliyeuwa kwa shambilio la risasi siku ya maandamano ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wameendamana kudai kuapishwa mawakala wao katika uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Kinondoni uliofanyika tarehe 19 Februari 2018.

Viongozi hao ni pamoja na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendedeleo (Chadema) Vicent Mashinji Katibu Mkuu wa (hadema), Salum Mwalim Naibu Katibu Chadema Zanzibar, John Mnyika Naibu Katibu Chadema Bara, Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini,

Siku ya tarahe 17 Februari 2018, majinzi na simanzi zilitawala kwa familia ya Mwanafunziwa Chuo (NIT) Akwelina baada ya kupigwa risasi iliyorushwa kwenye maandamano yaliyofanywa wafuasi wa chama cha Demokrasia eneo la Kinondoni Dar es Salaam waliokuwa wakidai usawa na uwapishaji kwa wakati kwa mawakala wao.

Tarehe 29 Desemba Mwaka 2018 Katibu Mkuu Mashinji na wafuasi wengine watatu alitiwa mbaroni na jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma zile zile zinazowakabili wapinzani za kufanya mkusanyiko usio kuwa halali.

Wengine waliokamatwa na Mashinji ni pamoja na Basil Lema, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Helga Mchomvu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai na Irine Lema na Msaidizi wa Mbunge wa Hai , Freeman Mbowe.

Siku ya ijumaa ya tarehe 23 mwezi Novemba imekuwa ngumu sana kwa Kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzani nchini Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Matiko kwa kiufutiwa dhamana yao kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kilichoelezwa kuwa wamekiuka Mashart ya Dhamana .

Leo ni siku ya 39 tangu Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri alipofuta dhamana ya viongozi hao ambapo wamesherehekea sikuu ya Krismasi wakiwa magereza, na hata mwaka utapinduka wakiwa magereza.

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo pia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe alitiwa mbaroni mara kadhaa ma jeshi la polisi alipokuwa kwenye harakati na wajibu wake kama mwanasiasa.

Tarehe 31 Oktoba mwaka 2018 Zitto alikamatwa na kuhojiwa kwenye kitou cha Polisi cha Osterbay kuhusu mauji ya raia wa kijiji ya Mpeta wilayani Uvinza mkoni kigoma ambapo alinyimwa zamana na kuhamishwa kwenye kitoa cha mburahati alikolala.

Tarehe 23 Februari Zitto alikamatwa akiwa mkoani Morogoro akiwa kwenye ziara ya chama ya kutembelea kata na halmashauri zinazoongozwa na chama chake.

Lakini yaliyoibua faraja na furaha ni pamoja na kuzinduliwa kwa mradi wa kufua umeme kwenye mto rufiji, Stiegler’s Gorge, mradi wa reli ya umeme, Standard gauge, kuzinduliwa kwa daraja la juu la Mfugale lililokuwepo Tazara jijini Dar es Salaam.

Mafanikio haya yote taifa limetwaa chini ya utawala wa Rais John Magufuli ambaye kwa sasa ameimarisha shirika la ndege kwa kununua ndege.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!