Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Michezo Messi, Ronaldo wamekosa nidhamu
Michezo

Messi, Ronaldo wamekosa nidhamu

Spread the love

KITENDO cha Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kutotokea kwenye hafla ya utoaji tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kimetafsiriwa kama utovu wa nidhamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Real Madrid, Fabio Capello amesema kitendo cha wawili hao tutotokea katika tuzo hizo ni utovu wa nidhamu au hawakubali kushindwa.

Kati ya hao wawili ni Ronaldo pekee ndiyo aliyebakia katika kinyang’anyiro hicho sambamba na Luka Modric ambaye alishinda tuzo hiyo na Mchezaji wa klabu ya Liverpool Mohammed Salah ambaye alishinda tuzo ya goli bora la mwaka alilofunga dhidi ya Everton.

Capello amesema kuwa kukosekana kwa wachezaji hao jana kunaonesha ni jinsi gani walivyowakosea heshima wapenzi na mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu ulimwenguni pamoja na wachezaji wenzao.

“Kukosekana kwa Messi na Ronaldo ni kuwakosea heshima wachezaji, FIFA na ulimwengu wa mpira wa miguu kwa ujumla, kwa kuwa wao wameshinda tuzo hii mara nyingi na hawapo tayari kushindwa, katika maisha unatakiwa kuwa vizuri ukishinda na hata kushindwa pia,” amesema Capello.

Modric ambaye ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka, umekuwa ni mwaka mzuri sana kwake baada ya mwezi juni kushinda tuzo ya mchezaji biora wa mashindano ya kombe la Dunia na barani Ulaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!