Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Saa 24 za kilichojiri Ukara  
Habari MchanganyikoTangulizi

Saa 24 za kilichojiri Ukara  

Spread the love

WAKATI harakati mbalimbali zikiendelea kufanywa na serikali kuhakikisha shughuli za wakazi wa Kisiwa cha Ukara zinaendelea, hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa. Anaripoti Mwandishi wetu…(endelea).

MV TEMESA yape jukumu

Meli ya Mv TEMESA imepewa jukumu lililokuwa la Meli ya MV Nyerere kwa kusafirisha abiria na mali zako kuanzia kesho tarehe 26 Septemba 2018.

Serikali imechukua hatua hiyo ili kuhakikisha wakazi wa kisiwa hicho wanaendelea na shughuli zao kama kawaida baada ya meli ya MV. Nyerere kuzama na kuangamiza Watanzania zaidi ya 226.

Mwili wa mtoto waopolewa

Wakati juhudi za kuiinua Meli ya Mv. Nyerere zikiendelea, leo tarehe 25 Septemba waokoaji wameopoa mwili wa mtoto.

Uopoaji huo umeenda sambamba na kuendelea kuopoa miili mingine iliyosaliwa kwenye meli hiyo wakati huu wazamiaji na wataalamu wakiendelea na juhudi za kuiinua meli hiyo.

Mizigo yaelea

Katika Ziwa Victoria ilipozama Meli ya Mv. Nyerere, mizigo mbalimbali ya wasafiri waliokuwemo kwenye meli hiyo imeanza kuelea.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mizigo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vifurushi, mabegi na nguo mali zlilizokuwa za wasafiri hao.

Baadhi ya mizigo hiyo imekuwa ikiopolewa kwa kuwa, imeelea karibu na kingo za Ziwa Victoria. Kazi hiyo inaendelea kusimamiwa na serikali.

Fedha zatolewa

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele ameanza kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni moja kwa waathiriwa wa ajali ya Mv. Nyerere.

Rais Magufuli jana alitoa ahadi ya kutoa kiasi hicho cha fedha leo ikiwa ni nje ya zile Sh. 500,000 zilizoahidiwa na serikali hapo awali. Utaratibu wa kugawa fedha hizo unaendelea kufanywa na Waziri Kamwele.

Kunyanyuliwa kivuko

Katika eneo lililotokea ajali, operesheni ya kuinyanyua Meli ya MV. Nyerere inayofanywa na wataalamu kutoka Kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na vikosi vya ulinzi na usalama imeanza kufanikiwa.

Wataalamu wamefanikiwa kuilaza ubavu meli hiyo ambapo kazi ya kuinyanyua meli hiyo bado inaendelea kufanywa na wataalamu hao kwa ufanisi na mafanikio makubwa.

Waziri Kamwelwe anasema, hatua iliyofikiwa katika unyanyuaji meli hiyo ni nzuri ambapo ubavu sasa unaonekana vizuri.

Mil 160 zakusanywa leo

Jumla ya Sh. 160.3 milioni zimechangwa na taasisi mbalimbali kwa lengo la kuhudumia waathirika wa ajali ya Mv. Nyerere. Michango hiyo imetolewa na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za dini, uvuvi, mabenki, makanisa na wananchi.

Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam limetoa Sh. 25 milioni, Benki ya KCB (Sh. 125 milioni), Benki ya Posta (Sh. 10 milioni), John Salia silingi 100,000 na Abel Michael shilini 200,000.

Leo Waziri Kamwelwe amesema, jumla ya michango yote tangua kuanza kupokewa imefika Sh. 557 milioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!