Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Shaffih Dauda atoka kwa dhamana, Soudy Brown aendelea kusota
Habari MchanganyikoTangulizi

Shaffih Dauda atoka kwa dhamana, Soudy Brown aendelea kusota

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachilia kwa dhamana watangazaji Sudi Kadio maarufu kama Soudy Brown na Shaffih Dauda na wengine wanne. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kwa wakati tofauti na mahakimu tofauti watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashataka yao kisha kuachiwa kwa dhamana. 

Mbele ya Hakimu Mfawidhi Kelvin Mhina Mshtakiwa Shaffih Dauda na Benedict Felix Kadege wasomewa shitaka moja kuchapisha maudhui kwenye televeshion ya mtandao bila kusajiliwa.

Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono amedai kuwa Dauda na Kadega wamekuwa wakichapisha maudhui kupitia televisheni ya mtandaoni ‘Youtube’ bila kusajiliwa na Mamlaka ya mawasilino nchini (TCRA).

Washtakiwa wamekana shitaka lao na mahakama kuwapa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh. 15 milioni kila mmoja sambasamba na washtakiwa kupewa sharti la kutosafiri nje ya nchi mpaka kwa ruhusa ya mahakama.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika ambapo hakimu Mhoina ameihailisha kesi hiyo mpaka tarehe 9 Oktoba mwaka huu.

Mbele ya Augostino Rwizile, Sudi Kadio ‘Soud Brown’ mtangazaji wa kipindi cha Shirawadu cha Clouds TV amesomewa shitka la kuendesha televisheni ya mtandaoni bila kusajiliwa na Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA).

Wakili wa Seriklai Mkuu Faraja Nguka alimsomea shitaka hilo Soudy Brown ambapo amedai kuwa mtuhumiwa kati ya tarehe 11 Juni na Septemba mwaka huu alichapisha na kumiliki televisheni ya mtandaoni inayojulikana kwa jina la Shirawadu TV bila kusajiliwa na TCRA.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, Soudy Brown alikana ambapo upande wa Jamhuri ulidai mahakamani hapo kuwa upelelezi haujakamilika.

Peter Kibatala wakili anayemtetea Soudy Brown aliiomba mahakama impe dhamana yenye masharti nafuu mteja wake huyo.

Hakimu Rwizile alimpa dhamana mtuhumiwa kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini bondi ya Sh. 2 milioni na yeye mwenyewe kujidhamini kwa kusaini bondi ya Sh. 2 milioni.

Kesi hiyo imehailishwa mpaka tarehe 18 Oktoba mwaka huu. Hata hivyo Jeshi la Polisi linaendelea kumshikiria Soudy Brown kwa madai ya kuwa anakesi nyengine ambapo linategemea kumpandisha tarehe 26 Septemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!