Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Simu ya JPM yampeleka Lukuvi Bunda
Habari za Siasa

Simu ya JPM yampeleka Lukuvi Bunda

Spread the love

SIKU 12 baada ya Rais John Magufuli kumwagiza William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutatua mgogoro wa kiwanja cha Nyasasi Masike, sasa ametua Bunda mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Utekelezaji wa utatuzi wa mgogoro huo upo ndani ya Kampeni ya “Funguka kwa Waziri wa Ardhi” inayoendeshwa na Waziri Lukuvi inayoanza leo tarehe 17 hadi 30 Septemba 2018.

Ziara hiyo imelenga kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mikoa minane ya Tanzania Bara katika wiki mbili mfululizo.

Lukuvu aliizindua rasmi mwezi Januari mwaka 2018 ikiwa na lengo la kuzunguka nchi nzima kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinazohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi papo hapo.

“Jumatatu ya leo tarehe 17 Septemba naanzia wilayani Bunda ili kutatua mgogoro wa Bibi Nyasasi Masike na kukagua kiwanja chake kama nilivyomuahidi Mheshimiwa Rais wakati alipofanya ziara yake wilayani Bunda na kunipigia simu moja kwa moja” Amesema Lukuvi na kuongeza;

“Nimeagizwa na Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano hii hadi kufikia 2020 migogoro ya ardhi iwe imepungua kwa kiasi kikubwa kama sio kuisha na kazi hii ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na ninawaagiza viongozi wajitokeze kuwasikiliza na kutafutia ufumbuzi kero za wananchi wanyonge ambazo zimekuwa zikiwatesa kwa muda mrefu.”

Tarehe 5 Septemba 2018 Rais Magufuli alimwagiza Lukuvi kufuatilia na kutatua mgogoro wa Bibi Nyasasi na kuhakikisha anamaliza mgogoro huo haraka.

Bibi Nyasasi akiwa na jirani yake walimlalamikia Rais Magufuli kuwa, kuna tajiri aliyedhulimu kiwanja chake baada ya kumuuzia kiwanja cha pili kwa ajili ya kupata fedha za matibabu, na kwamba aliporudi kutoka kupata matibabu alikuta tajiri huyo amejimilikisha kiwanja cha pili.

Kwenye kampeni hiyo ya wiki wiki mbili, Lukuvi atatatua migogoro ya ardhi katika mikoa minane na kuanzia tarehe 17 hadi 19 atakuwa katika Mkoa wa Mara katika Wilaya ya Bunda, Musoma na Tarime na baadaye tarehe 20 hadi 30 atakuwa katika Mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Njombe, Iringa na Morogoro.

Wakati wa utatuzi wa mgogoro wa Bibi Nyasasu, Lukuvi pia atasikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu sekta ya ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mkutano wa hadhara utaofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!