March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kalanga ashinda Monduli, aahidi makubwa

Spread the love

MBUNGE mteule katika jimbo la Monduli aliyeshinda kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika jana tarehe 16 Septemba 2018 kwa kura asilimia 95, Julius Kalanga ameahidi kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zilizomo kwenye jimbo hilo, hasa migogoro ya ardhi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kalanga ametoa ahadi hiyo baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo na Msimamizi wa Uchaguzi Monduli, Steven Ulaya usiku wa kuamkia leo tarehe 17 Septemba 2018.

“Napenda kuchukua fursa hii kukishukuru Chama cha Mapinduzi CCM na mwenyekiti wake na wanachama pamoja na wananchi wa jimbo hili tulioshirikiana nao katika jambo hili. Nashukuru tulifanya kampeni za kistaarabu jimbo letu limebaki na amani,” amesema na kuongeza Kalanga.

“Yako mambo ya msingi tuliyokubaliana na wananchi nilioingia nao mkataba, wananchi waliniamini walinipa kura yao. Yako mambo ya msingi ya kufanya, jambo la kwanza ni maji, maeneo mengi ni kame, pili nitrashirikiana na serikali ili kutafutia ufumbuzi, kuondoa migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda wa miaka 20 kutafutia ikiwemo kubainisha mipaka.”

Katika uchaguzi huo, Kalanga alichuana na Yonas Laizer wa Chadema aliyepata kura 3,187 ,Wilfred Mlay wa ACT Wazalendo  (144), Feruz Juma wa NRA (45), Simon Ngilisho wa Demokrasia Makini (35), Omary Juma wa DP (34), mgombea wa ADA-Tadea, Francis Ringo (21) na Elizabeth Salewa wa chama cha Wakulima aliyepata kura 16.

error: Content is protected !!