Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwita Waitara arudi tena Ukonga
Habari za Siasa

Mwita Waitara arudi tena Ukonga

Mwita Waitara, Naibu wa Waziri wa TAMISEMI
Spread the love

MGOMBEA Ubunge wa CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Ukonga uliofanyika jana, Mwita Waitara ameibuka mshindi baada ya kupata kura ya asilimia 89.1. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Waitara ametangazwa mshindi leo tarehe 17 Septemba 2018 na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Ukonga, Jumanne Shauri, ambapo msimamizi huyo alisema Waitara alipata kura 77,795.

Katika uchaguzi huo, mpinzani wa karibu alikuwa mgombea wa Chadema, Asia Msangi aliyeambulia kura 8,676 sawa na asilimia 9.95.

Wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Shauri alisema waliopiga kura ni asilimia 29.4 kati ya watu 300,609 ya waliotarajiwa kupiga kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wananchi Dar watakiwa kujitokeza barabarani kumuaga Hayati Mwinyi

Spread the loveWANANCHI wasiokuwa na muda wa kwenda katika Uwanja wa Uhuru,...

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

error: Content is protected !!